• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kibaha District Council
Kibaha District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

  • Mwanzo
    • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • SP FINAL DRAFT
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasmali Watu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Usimamizi wa Sheria
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sehemu ya Mifugo
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uchumi na Mipango
      • Maadili
      • UKIMWI
      • Huduma za Jamii
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

WWF YAKABIDHI MICHE YA MICHIKICHI KUHIFADHI KINGO ZA MTO RUVU

Posted on: May 24th, 2025

Katika kuimarisha uhifadhi wa mazingira ya Mto Ruvu, Shirika lisilo la kiserikali la WWF limekabidhi miche 2,500 ya michikichi kwa vikundi vya kijamii katika vijiji vya Mwembengozi, Kimaramisale na Kitomondo Ruvu, Halmashauri Wilaya ya Kibaha.


Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bi. Evelyne Ngwira, aliwashukuru WWF na Bodi ya Maji Bonde la Ruvu kwa ushirikiano wao katika kutekeleza mradi huo wa kilimo hifadhi. Alieleza kuwa hadi sasa zaidi ya ekari tano zimepandwa michikichi na kusisitiza matumizi ya wataalamu wa kilimo kwa tija ya zao hilo.


Bi. Ngwira alisema michikichi husaidia kuhifadhi mazingira, huku pia ikiwa chanzo cha mafuta, sabuni, kuni na kipato kwa familia.


Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Afisa Tarafa wa Ruvu, Bi. Roina Ilomo, aliwataka wanavikundi kuhakikisha miche inatunzwa ipasavyo ili kufikia malengo ya mradi.


Kwa mujibu wa Mratibu wa Mradi kutoka WWF, Eng. John Kasambili, miche hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mafunzo ya utunzaji mazingira yaliyotolewa kwa wanavikundi.


Mradi huu ni sehemu ya Mradi wa Usalama wa Maji kwa Jiji la Dar es Salaam na Mijiji ya Pembezo, unaofadhiliwa na kampuni ya ABInBeV/TBL, uliyozinduliwa mwaka 2022 na Naibu Waziri wa Maji, Mh. Maryprisca Mahundi.


Kupitia mradi huo, tayari miche 2,200 imepandwa katika vijiji vya Ruvu Station, Minazimikinda na Kitomondo; mizinga 45 na miche rafiki wa maji 20,000 imetolewa kwa vijiji 9 vya Kibaha na Kisarawe, sambamba na ujenzi wa miundombinu ya maji na uboreshaji wa takwimu za ubora wa maji ya Mto Ruvu.


Aidha, ukarabati wa bwawa la Kiembaemba unatarajiwa kuanza Julai 2025.

Matangazo

  • MAONESHO YA NANE NANE KANDA YA MASHARIKI YANATARAJIWA KUANZA RASMI TAREHW 01.08.2025 WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA July 18, 2025
  • Tarehe 31.07.2025 MHESHIMIWA RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN ATAZINDUA BANDARI KAVU YA KWALA WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA July 28, 2025
  • Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuzindua bandari kavu Kwala tarehe 31.07.2025 July 25, 2025
  • Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuzindua bandari kavu Kwala tarehe 31.07.2025 July 25, 2025
  • Angalia Vyote

Matukio mapya

  • KWALA YAANDIKA HISTORIA MPYA, RAIS SAMIA AZINDUA SAFARI ZA MIZIGO SGR NA BANDARI KAVU MKOANI PWANl

    July 31, 2025
  • KWALA YAANDIKA HISTORIA MPYA: BANDARI KAVU, VIWANDA NA TRENI YA MIZIGO KUZINDULIWA NA RAIS SAMIA KESHO

    July 30, 2025
  • MANAGEMENT YA HALASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA YATEMBELEA BANDARI KAVU KWALA

    July 28, 2025
  • MANAGEMENT YA HALASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA YATEMBELEA BANDARI KAVU KWALA

    July 28, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Kuzindua bunge
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TOVUTI YA MKOA WA PWANI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA AJIRA
  • TOVUTI YA WANANCHI
  • TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI
  • TOVUTI YA WIZARA YA AFYA
  • TOVUTI YA EWURA

Tovuti Zinazoshabihiana

  • TAMISEMI
  • MKOA WA PWANI
  • TANZANIA
  • AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    KIBAHA DISTRICT COUNCIL

    Anwani ya Posta: P.O BOX 30153

    Simu ya Mezani: +255 23240224

    Simu: +255 0767520048

    Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM)
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.