• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kibaha District Council
Kibaha District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

  • Mwanzo
    • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • SP FINAL DRAFT
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasmali Watu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Usimamizi wa Sheria
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sehemu ya Mifugo
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uchumi na Mipango
      • Maadili
      • UKIMWI
      • Huduma za Jamii
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Historia ya Wilaya

1.0: JIOGRAFIA YA WILAYA

1.1: Mipaka Na Eneo 

Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha iko umbali wa kilometa 40 toka Jiji la Dar es salaam kando kando ya barabara kuu iendayo Morogoro. Halmashauri ya Wilaya inapatikana kati ya latitudi 6-8 Kusini mwa Ikweta na Longitudi 38.0 hadi 39.05 Mashariki. Kaskazini inapakana na Wilaya ya Bagamoyo, na Kusini inapakana na Wilaya ya Kisarawe, upande wa Mashariki inapakana na Halmashauri ya Mji wa kibaha, Upande wa Magharibi inapakana na Wilaya ya Bagamoyo na Wilaya ya Morogoro.

1.2: Utawala / Eneo

Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha ina jumla ya Tarafa 2 na Kata 14. Tarafa ni Mlandizi na Ruvu,Kata zake ni Kwala, Ruvu, Magindu, Mlandizi, Soga, Janga, Kilangalanga, Gwata, Bokomnemela, Dutumi, Kikongo, Kawawa, Mtongani, na Mtambani. Ikiwa na jumla ya Vijiji 25 na Vitongoji 100. Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha ina eneo la ukubwa wa Hekta 124,217.755 sawa na kilometa za mraba 1992.18

 

1.3: Mipaka                

Halmashauri ya Wilaya inapatikana kati ya latitudi 6-8 Kusini mwa Ikweta na Longtudi 38.0 hadi 39.05 Mashariki. Kaskazini inapakana na Wilaya ya Bagamoyo, na Kusini inapakana na Wilaya ya Kisarawe, upande wa Mashariki inapakana na Halmashauri ya Mji wa kibaha, Upande wa Magharibi inapakana na Wilaya ya Bagamoyo na Wilaya ya Morogoro.

1.4: Idadi Ya Watu

Kwa mujibu wa Sensa ya  watuna makazi mwaka 2012, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha ina jumla ya Kaya 17,124 na watu wapatao 70,209 ikiwa ni ongezeko la asilimia 2.2 Jedwali lifuatalo linaonyesha mchanganuo wa idadi ya watu katika kila Kata kijinsi, wastani kwa kaya na uwiano kijinsia.

JEDWALI NA. 1:  IDADI YA WATU KWA KATA 

KATA

JUMLA YA WATU

ME

KE

WASTANI KWA KAYA

UWIANO KIJINSIA

Gwata

5,280

2,585

2,695

4.7

96

Dutumi

1,812

939

873

4.2

108

Magindu

4,991

2,453

2,538

4.5

97

Soga

4,713

2,428

2,285

3.7

106

Kikongo

4,238

2,112

2,126

3.7

99

Ruvu

3,466

1,719

1,747

3.8

98

Mlandizi

17,318

8,546

8,772

4.2

97

Kwala

3,472

1,749

1,723

3.8

102

Kilangalanga

10,588

4,997

5,591

4.3

89

Janga

10,926

5,242

5,684

4.0

92

Bokomnemela

3,405

1,745

1,660

3.8

105

Total 

70,209

34,515

35,694

4.1

97

Chanzo: Sensa ya Watu na Makazi Tanzania, 2012.

 

1.5: Hali ya Hewa

Wilaya ina misimu miwili ya mvua, Vuli miezi ya Novemba na Desemba na Masika miezi ya Machi hadi Aprili. Wastani wa mvua kwa mwaka ni mm 800. Wastani wa joto ni nyuzi joto 29.7 na wastani wa unyevu unafikia 56%.

 

3.0: HALI YA MAENDELEO YA HALMASHAURI YA WILAYA

3.1: Hali ya kiuchumi na kijamii

Halmashauri ya Wilaya Kibaha ina wakazi wachache waliosambaa katika maeneo mbalimbali isipokuwa Mji wa Mlandizi wenye wakazi wengi. Mji wa Mlandizi unakua haraka ukiwa na watu wa Tabaka mbalimbali na tamaduni zinazotofautiana. Ukaribu wake kutoka Mji Mkuu wa kibiashara Dar es Salaam unachangia kwa kiasi kikubwa. Mabadiliko ya kijamii na kiutamaduni hasa kutoka nchi za Kimagharibi.

Mlandizi inazo Taasisi nyingi za Umma na Binafsi zinazosaidia kutoa ajira kwa wakazi.  Hizi ni pamoja na shule za Msingi na Sekondari, JKT na Idadi kubwa ya wafanyabiashara kama maduka ya jumla, rejareja, migahawa, mama lishe vilabu vya pombe za kienyeji, viwanda vidogo kama upasuaji wa mbao, ushonaji, usagishaji n.k.

Shughuli za kiuchumi katika Halmashauri ya wilaya Kibaha ni kilimo, ufugaji ukiendeshwa zaidi na makabila ya Kimasai na Mang’ati hususani katika Kata za Kwala na Magindu. Ipo idadi ndogo ya wakazi wanaoendesha ufugaji wa kisasa wa kuku na ng’ombe wa maziwa. Mazao makuu ya kilimo ni Korosho, Ufuta, Machungwa, kilimo cha mbogamboga kama Matango, Nyanya, Pilipilli, Bilinganya, Matikiti maji n.k, kwa asilimia kubwa kilimo hiki hufanyika katika Bonde la Mto Ruvu. Mazao ya chakula ni pamoja na Mhogo, Mpunga, Mtama na Mahindi.

Shughuli za kilimo kwa kiasi kikubwa ni kwaajili ya kujikimu kwa chakula, ni watu wachache tu, hususani Mlandizi wako waajiriwa katika Taasisi za Umma na Binafsi kwa shughuli hii. Baadhi ya wakazi wanajishughulisha na uvunaji wa mazao ya Misitu kwa ajili ya ujenzi, kuni na uchomaji mkaa, kwa kiwango kidogo pia hujishughulisha na ufugaji na uvunaji wa mazao ya nyuki.

Huduma za jamii zinazopatikana ni Afya, Elimu, Maji na Barabara. Mafanikio yote haya ni juhudi zinazofanywa na Halmashauri ya Wilaya Kibaha.

15.0: MWISHO

Kwa mujibu wa taarifa hii, Wilaya imekuwa na mafanikio ya kuridhisha katika kuboresha hali ya maisha ya wananchi wake kupitia utoaji wa huduma za Kijamii za Elimu, Afya, Maji na huduma za kiuchumi za Barabara, Madaraja, Majengo; Kilimo, Uvuvi, Mifugo, Utalii, Biashara, Mawasiliano na Ardhi.  Aidha, huduma ya Utawala bora imeongezeka pamoja na kudumisha hali ya amani, ulinzi na usalama wa raia na mali zao.  Mafanikio haya yametokana na ushirikiano mzuri baina ya uongozi wa Chama na Serikali Wilayani, watendaji wa Wilaya, Taasisi, Wananchi na Wadau mbalimbali Wa Maendeleo hapa wilayani Kibaha.

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI WA BVR HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA January 23, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • MABADILIKO YA TAREHE YA USAILI September 24, 2024
  • Angalia Vyote

Matukio mapya

  • KAIMU KATIBU TAWALA WILAYA YA KIBAHA ATOA WITO KWA WENYEVITI WA MJI MDOGO MLANDIZI KUZINGATIA UADILIFU

    February 11, 2025
  • MAKAMU WA RAIS AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, ATOA WITO DHIDI YA UBADHILIFU

    April 02, 2025
  • ELIMU YA LISHE JUU YA USINDIKAJI WA BIDHAA ZA VYAKULA YATOLEWA KIBAHA DC.

    March 23, 2025
  • Mwenyekiti wa Halmashauri Amshukuru Rais Samia kwa Fedha za Miradi

    February 05, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Kuzindua bunge
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TOVUTI YA MKOA WA PWANI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA AJIRA
  • TOVUTI YA WANANCHI
  • TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI
  • TOVUTI YA WIZARA YA AFYA
  • TOVUTI YA EWURA

Tovuti Zinazoshabihiana

  • TAMISEMI
  • MKOA WA PWANI
  • TANZANIA
  • AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    KIBAHA DISTRICT COUNCIL

    Anwani ya Posta: P.O BOX 30153

    Simu ya Mezani: +255 23240224

    Simu: +255 0767520048

    Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM)
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.