• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kibaha District Council
Kibaha District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

  • Mwanzo
    • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • SP FINAL DRAFT
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasmali Watu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Usimamizi wa Sheria
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sehemu ya Mifugo
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uchumi na Mipango
      • Maadili
      • UKIMWI
      • Huduma za Jamii
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mipango na Uratibu

Utekelezaji Idara ya Mipango na Uratibu

Idara ya mipango na takwimu inajumuisha wataalamu wa mipango na takwimu ambao kwa ujumla wanasimamiwa na Afisa mipango wa wilaya. Idara ya mipango ndiyo inayoratibu shughuli zote za miradi ya maendeleo pamoja na kuandaa taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi hiyo mfano taarifa za robo mwaka, taarifa za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi, uratibu wa uandaaji wa bajeti na utekelezaji wake,  n.k. Taarifa hizi hupelekwa ngazi za juu kwa ajili ya ufuatiliaji zaidi.

Majukumu ya idara hii kiutawala yameainishwa kuonesha majukumu ya mtakwimu na majukumu ya wachumi/mipango ila katika utekelezaji majukumu haya hutekelezwa kwa pamoja. Pamoja na kuahinishwa kwa majukumu hayo, pia Idara kwa mujibu wa waraka mpya wa muundo wa Idara za Halmashauri, Idara ina sehemu kuu tatu;

  • Sera na Mipango (Policy and Planning),
  • Tathamini na Ukaguzi wa Miradi (Monitoring and Evaluation),
  • Takwimu (Statistics)

Majukumu ya Mipango (Sera na Mipango & Tathmini na Ukaguzi wa Miradi)

Kuratibu masuala yote ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Kuandaa mpango na taarifa za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha tawala kwa kipindi cha miaka mitano,mwaka mmoja na nusu mwaka.

      Kufanya tathmini na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ili kubaini ubora wa mradi na thamani ya fedha iliyotolewa (value for money)

      Kuratibu miradi iliyofadhiliwa na Wahisani wilayani.

      Kuratibu Mipango na Bajeti ikiwemo Mpango Mkakati na Mipango kazi ya wilaya.

      Kuunganisha, kuratibu na kufuatilia Mipango na Bajeti za Serikali za mitaa.

     Kushiriki katika kufuatilia, kukagua na kutoa tathmini kwenye miradi ya maendeleo wilayani ili kupata takwimu sahihi za utekelezaji wa kazi za serikali.

     Kushiriki katika kuandaa taarifa za utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo.

     Kuratibu shughuli za tafiti zote wilayani, ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti za kina kuhusu vyanzo vya mapato vya Halmashauri.

Kuchapisha machapisho mbalimbali ya kiucumi na kijamii wilayani.

Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa mkataba wa huduma kwa wateja.

Idara ya Mipango ndiyo Sekretarieti katika vikao vya Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC).

Kuratibu masuala ya Maafa katika wilaya.

Kazi Za Mtakwimu Wa Halmashauri

Mtakwimu wa Halmashauri anashiriki katika kazi zote za kitakwimu zinazofanyika katika halmashauri. Mtakwimu anafanya kazi chini ya usimamizi wa Afisa Mipango Wilaya. Kazi za mtakwimu wa wilaya ni kama ifuatavyo;

  1. Kusimamia kitengo vya Takwimu katika Halmashauri Kukusanya, kuchambua, kutafsiri na kuwasilisha takwimu ili ziweze kutumika katika mipango ya Halmashauri.

Kushirikiana na idara zote za kisekta (kwa mafano Afya, Elimu, Kilimo, n.k) ndani ya Halmashauri ili kuwa na mfumo mzuri wa kitakwimu.

Kuandaa mkusanyiko wa takwimu za kiuchumi na kijamii“(Socio economic profile),

Kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakati wa zoezi la Sensa ya idadi ya watu na Makazi.

Mtakwimu pia ni mwenyekiti wa kikundi kazi cha ukusanyaji wa takwimu ndani ya Halmashauri (District Statistics Working Group).

Kufuatilia mwenendo wa mfumo wa utunzaji wa takwimu katika ngazi ya serikali za mitaa(LGMD) na kushirikiana na idara nyingine zenye mifumo mingine ya utunzajia wa takwimu za kisekta kwa mfano;

Maliasili - NAFOBEDA, Afya - MTUHA na Elimu - BEST.

LGMD - Local Government Monitoring database, BEST-Basic Education Statistics na NAFOBEDA - National Forestry and Beekeeping Database.

JEDWALI NA. UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU IDARA YA MIPANGO

NA.

UTEKELEZAJI

Utekelezaji kwa Vitengo vya Mipango & Sera; Mipango & Tathmini na Ukaguzi wa Miradi


Kuratibu masuala ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Idara imekuwa ikishirikiana na Idara zingine kuboresha na kuinua maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa kuendelea kuboresha miradi ya maendeleo.

Kuandaa Mpango na Taarifa za Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha Miaka mitano, mwaka mmoja na nusu mwaka.
Taarifa ya Utekelezaji Ilani ya Chama kwa kipindi cha cha mwaka mmoja na ile ya Miaka mitano zote huandaliwa na kuwasilishwa Mkoani, ambapo Taarifa ya Miaka Mitano iliwasilishwa kwa barua yenye KUMBUKUMBU NA. KDC/A. 160/41/39 ya tarehe 06 August, 2015.

Kufanya tathmini na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ili kubaini ubora wa mradi na thamani ya fedha iliyotolewa (value for money).
Idara kwa kushirikiana na Idara za Maji, Kilimo, Mifugo na Ujenzi, hufanya ziara za ukaguzi katika miradi yote. Miradi iliyokaguliwa ipo kwenye ubora unaotakiwa.

Kuratibu miradi iliyofadhiliwa na Wahisani wilayani.
Idara hutekeleza uratibu wa miradi inayofadhiliwa na wahisani kwa kushirikiana na Idara husika.

Kuratibu Mipango na Bajeti ikiwemo Mpango Mkakati na Mipango kazi ya wilaya.
Bajeti, Mpangomkakati, pamoja na Mpangokazi wa Halmashauri huandaliwa kwa wakati na kuwasilishwa mamlaka za juu kwa mujumuisho ya kitaifa. Kwa sasa utekelezaji wake unaendelea. Aidha, mchakato wa Bajeti, Mpangomkakati, na Mpangokazi kwa mwaka mpya wa fedha wa 2016/17 upo katika hatua za mwisho.

Kuunganisha, kuratibu na kufuatilia Mipango na Bajeti za Serikali za mitaa.
Ufuatiliaji unafanyika na utekelezaji unaendelea

Kushiriki katika kufuatilia, kukagua na kutoa tathmini kwenye miradi ya maendeleo wilayani ili kupata takwimu sahihi za utekelezaji wa kazi za serikali.
Ufuatiliaji ni jukumu endelevu ambapo hufanyika kwa kila mwisho wa robo mwaka, miradi inakaguliwa na taarifa huwa zinawasilishwa ofisi ya mkurugenzi.

Kushiriki katika kuandaa taarifa za utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo.
Maandalizi ya taarifa kwa vipindi vya robo mwaka hufanyika na taarifa kuwasilishwa kwenye kikao cha Kamati za kudumu kwa mujibu wa sheria katika kikao cha tarehe 21 Oktoba, 2015.

Kuratibu shughuli za tafiti zote wilayani, ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti za kina kuhusu vyanzo vya mapato vya Halmashauri.
Mpaka sasa tafiti zilizofanyika ni pamoja na tafiti ndogo za vyanzo vya mapato katika ushuru wa;
  • Mchanga; Tumejiridhisha kuwa Halmashauri inaweza kuingiza jumla ya sh. 225,720,000.00.
  • Soko; Tumejiridhisha kuwa Halmashauri inaweza kuingiza jumla ya sh. 31,140,000.00.
  • Stendi; Tumejiridhisha kuwa Halmashauri inaweza kuingiza jumla ya sh. 131,400,000.00.
Aidha, Idara bado inaendelea kufanya tafiti kwa vyanzo vilivyobaki na utafiti wa njia bora ya kukuza mapato. Taarifa hizi zitakuwa zikiwasilishwa kwenye vikao kwa mujibu wa taratibu. Idara pia ipo kwenye mchakato wa kufanya tafiti ya jinsi ya kuwezesha uwekezaji wa pamoja kati ya Halmashauri na Sekta binafsi (PPP), pia utafiti wa kuanisha vikwazo na fursa zilizopo katika sekta ya uwekezaji, tafiti ya kuiwezesha sekta isiyorasmi kuchangia pato la halmashauri, na tafiti zingine kadiri itakavyoibuliwa kwa siku zijazo.

Kuchapisha machapisho mbalimbali ya kiucumi na kijamii wilayani.
Zoezi la uandaaji machapisho linaendelea. Kwa sasa Idara inajiandaa kuhuisha taarifa za machapisho ya ‘Council Socio-Economic Profile’ na ‘Council Investment Profile’.

Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa mkataba wa huduma kwa wateja.
Zoezi la kuhuisha Mkataba wa Huduma kwa Wateja hufanyika kwa kushirikiana na Idara ya Utumishi.

Idara ya Mipango ndiyo Sekretarieti katika vikao vya Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC).
Jukumu hili hufanyika kama utaratibu unavyoelekeza.

Kuratibu masuala ya Maafa katika wilaya.
Jukumu hili hufanyika kama utaratibu unavyoelekeza.

Utekelezaji kwa Kitengo cha Takwimu Wa Halmashauri

1.
Kusimamia kitengo cha Takwimu katika Halmashauri Kukusanya, kuchambua, kutafsiri na kuwasilisha takwimu ili ziweze kutumika katika mipango ya Halmashauri.
Zoezi la ukusanyaji takwimu linaendelea tatizo kubwa ni uhaba wa fedha. Idara inashauri kuwa, ruzuku kutoka serikali kuu na fedha za wahisani ziwe zinafika kwa wakati.
2.
Kushirikiana na idara zote za kisekta (kwa mafano Afya, Elimu, Kilimo, n.k) ndani ya Halmashauri ili kuwa na mfumo mzuri wa kitakwimu.
Zoezi la ukusanyaji takwimu linaendelea tatizo kubwa ni uhaba wa fedha. Idara inashauri kuwa, ruzuku kutoka serikali kuu na fedha za wahisani ziwe zinafika kwa wakati.
3.
Kuandaa mkusanyiko wa takwimu za kiuchumi na kijamii“(Socio economic profile).
Taarifa za awali zilizokusanywa ni pamoja na ‘Socio-Economic Profile’ na ‘Investment Profile’. Idara inaendelea na kuzihuisha takwimu hizi ili ziweze kuingizwa katika mfumo wa serikali kwa matumizi ya ngazi za juu. Zoezi linatekelezwa kwa kusua kusua kutokana na uhaba wa fedha. Idara inashauri kuwa, ruzuku kutoka serikali kuu na fedha za wahisani ziwe zinafika kwa wakati.
4.
Kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakati wa zoezi la Sensa ya idadi ya watu na Makazi.
Zoezi hili hufanyika kila baada ya miaka 10, mara ya mwisho lilifanyika 2012 hivyo litafanyika tena 2022.
5.
Mtakwimu pia ni mwenyekiti wa kikundi kazi cha ukusanyaji wa takwimu ndani ya Halmashauri (District Statistics Working Group).
Hatuna Kikundi kazi cha aina hii katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.
6.
Kufuatilia mwenendo wa mfumo wa utunzaji wa takwimu katika ngazi ya serikali za mitaa (LGMD) na kushirikiana na idara nyingine zenye mifumo mingine ya utunzajia wa takwimu za kisekta
Zoezi halijafanyika kutokana na ukosefu wa fedha.
Utekelezaji wa majukumu mengine
1
Maagizo kutoka serikali kuu
Idara imekuwa ikitekeleza maagizo yote kutoka serikali kuu moja kwa moja, maagizo yatokanayo na ziara za viongozi wa kitaifa na Maagizo yatokanayo na hotuba mbalimbali za viongozi. Taarifa zake huandaliwa na kuwasilishwa kwa Katibu Tawala (M).
2
Maagizo ya Mkurugenzi
Maagizo ya Mkurugenzi yanatokana na maazimio ya vikao mbalimbali vya kamati za kudumu za waheshimiwa madiwani, hivyo Idara imekuwa ikitekeleza kadiri inavyowasilishwa.




Changamoto

Changamoto kubwa inayoikabili Idara ni uhaba wa fedha, ambapo idara inaendelea na kuandika maandiko ya kutafuta fedha zitakazosaidia utekelezaji wa miradi. Maandiko hayo ni pamoja na uuzwaji wa hatifungani za halmashauri.

Malengo Ya Baadae

Pamoja na utekelezaji wa majukumu hayo, Idara ina malengo ya kutekeleza yafuatayo kadiri ya upatikaji wa fedha;

  • Kufanya tafiti kubwa za uwekezaji ili kuvutia wawekezaji katika sekta zote,
  • Kufanya tafiti za ukuzaji mapato ya ndani,
  • Kuandika maandiko ya miradi ya Ujenzi wa Soko, Ujenzi wa Stendi, Majengo ya Kibiashara, n.k.
  • Kuwezesha uuzwaji wa Hatifungani za Halmashauri ili kuharakisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo,
  • Kuwezesha ufanyikaji wa kongamano la kuinadi halmashauri kwa wawekezaji na vyombo vya habari,
  • Kuwezesha ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri na Ofisi ya Mji Mdogo wa Mlandizi,
  • Kubuni maeneo ya utalii na kuyatangaza,
  • Na kuendelea kuwezesha uboreshaji wa miundombinu ya kiuchumi.

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI WA BVR HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA January 23, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • MABADILIKO YA TAREHE YA USAILI September 24, 2024
  • Angalia Vyote

Matukio mapya

  • KAIMU KATIBU TAWALA WILAYA YA KIBAHA ATOA WITO KWA WENYEVITI WA MJI MDOGO MLANDIZI KUZINGATIA UADILIFU

    February 11, 2025
  • MAKAMU WA RAIS AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, ATOA WITO DHIDI YA UBADHILIFU

    April 02, 2025
  • ELIMU YA LISHE JUU YA USINDIKAJI WA BIDHAA ZA VYAKULA YATOLEWA KIBAHA DC.

    March 23, 2025
  • Mwenyekiti wa Halmashauri Amshukuru Rais Samia kwa Fedha za Miradi

    February 05, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Kuzindua bunge
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TOVUTI YA MKOA WA PWANI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA AJIRA
  • TOVUTI YA WANANCHI
  • TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI
  • TOVUTI YA WIZARA YA AFYA
  • TOVUTI YA EWURA

Tovuti Zinazoshabihiana

  • TAMISEMI
  • MKOA WA PWANI
  • TANZANIA
  • AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    KIBAHA DISTRICT COUNCIL

    Anwani ya Posta: P.O BOX 30153

    Simu ya Mezani: +255 23240224

    Simu: +255 0767520048

    Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM)
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.