Wakulima wa zao la korosho katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha wameomba serikali kuwatafutia suluhisho la wizi wa korosho kwani wamekuwa wakipata hasara kutokana na korosho nyingi kuokotwa na wezi.
Wakulima hao wametoa ombi hilo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Butamo Ndalahwa alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa zoezi la kugawa viwatilifu vya zao la korosho ambavyo vimetolewa bure kwa wakulima wa korosho ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo hapa nchini.
Moses Benard Mtandala ni mkulima wa zao la korosho amesema wamekuwa wakitumia gharama kubwa kuandaa mashamba na kuhudumia kosrosho lakini kipindi cha mavuno hawapati chochote kwani wezi huingia mashambani na kuokota korosho usiku na kwenda kuwauzia kangomba ( wabanguaji wa mtaani) Hivyo mkulima huyo alitoa ombi kwa serikali kuthibiti biashara ya kangomba badala yake kosrosho zote zipelekwe ghalani
Akiongea kwenye ziara hiyo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya kibaha Butamo Ndalahwa amewapongeza maafisa ugani kwa kusimamia vizuri zoezi la kugawa viwatilifu hivyo na kuwataka wakulima wa korosho kuhakikisha wanauza korosho zao katika mfumo wa stakabadhi ghalani na kuacha kuuza kwa kangomba hii itawasaidia kupata mgao mkubwa wa viwatilifu kwa mwaka unaofuta
Aidha Afisa Kilimo wa Wilaya eveline Ngwira alisema walipokea jumla ya mifuko 6750 ya sulpher pamoja na dawa za maji (indazole25-sc) lita 576 ambazo zimegawiwa kwa wakulima wa korosho waliosafisha mashamba .
Eveline aliongeza kuwa viwatilifu viligawiwa kwa wakulima walosafisha mashamba tu hivyo kuwataka wakulima wengine kusafisha mashamba yao ili waweze kupata viwatilifu kwa awamu I nayofuata
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.