RCKunenge atatua Mgogoro ardhi Kikongo Kibaha DC
Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ametatua mgogoro wa ardhi baina ya mwekezaji Trans Continental na wananchi wa kata ya Kikongo Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.
Wananchi 214 wa Kata ya Kikongo walilikuta eneo la mwekezaji huyo ambae alikuwa anamiliki ene hilo kihalali tangu mwaka 1987 na kuanza kufanya uendelezaji makazi kinyume na sheria.
Kunenge ametoa maamuzi hayo leo Oktoba 30, 2023 kwenye mkutano wa hadhara uliowahusisha Katibu Tawala wa mkoa, wananchi, watalaam wa halmashauri na mkoa.
Amesema hatua hiyo imetokana na jitihada za serikali kutafuta ufumbuzi wa migogoro inayowakabili wananchi.
“Mnatakiwa kufahamu kwamba eneo hili ni mali ya mwekezaji, mmelivamia sasa kwa busara nimemuomba mwekezaji awamegee eneo muanzishe makazi yenu kama kuna mtu hajaridhika anaweza kufuata sheria,” amesema Kunenge.
Mwekezaji wa shamba shamba namba 30/1 Abdrahim Zahran amekubali ombi la Mkuu wa mkoa kutoa eneo kwa ajili ya wananchi waliovamia shamba lake ambapo kila mwananchi atapewa eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 500.
Kuhusu eneo kwa ajili ya wananchi hao, amesema watagawa kulingana na vipaumbele vyao kwa sababu wamepanga kufanya uwekezaji wa miradi mingine.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.