HALMASHAURI ya Wilaya ya Kibaha inatarajia kuanza oparesheni sehemu za biashara kubaini kama kuna wafanyabiashara hawana leseni wapatiwe.
Hayo yameelezwa wakati wa kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo ambao wamesema kwa kufanya hivyo itasaidia kuongeza mapato.
Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha Erasto Makala alisema oparesheni hiyo itakuwa ni endelevu na kwamba timu ya mapato itashiriki moja kwa moja.
Makala alisema lengo la oparesheni hiyo ni kuhakikisha wanaongeza makusanyo ya mapato kupitia leseni za biashara.
"Katika oparesheni hii wale wafanyabiashara ambao hawana leseni wtapatiwa na fedha zitakazopatikana hapa zitasaidia kuondoa vikwazo vinavyosababishwa na ukosefu wa fedha" alisema.
Aidha Mwenyekiti huyo alisema kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023 hakutakuwa na chaguo la pili kwani kwasasa wameanza kusimamia ujenzi wa vyumba vya madarasa kulingana na fedha waliyopata.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Butamo Ndalawa alisema wamepokea sh. miln 340 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 17 ili kuwezesha wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2023 wote kupata nafasi.
Katika maeneo ambayo yanadaiwa kuwa na vikwazo vya upungufu wa vyumba vya madarasa Ndalawa aliwashauri Madiwani kuwahamasisha wananchi kushirikishwa kuchangia kuanza ujenzi na Serikali itatenga fedha kukamilisha.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.