• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kibaha District Council
Kibaha District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

  • Mwanzo
    • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • SP FINAL DRAFT
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasmali Watu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Usimamizi wa Sheria
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sehemu ya Mifugo
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uchumi na Mipango
      • Maadili
      • UKIMWI
      • Huduma za Jamii
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mwenge wa Uhuru 2024 Umekagua na kuzindua Miradi 13 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

Posted on: May 1st, 2024

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godfrey Mzava amesisitiza matumizi ya mfumo wa kidigitali katika kuwapata wazabuni kwenye miradi mbalimbali na kuondoa malalamiko kwa waombaji.


Amesema Serikali imeendelea kutoa fedha nyingi kwenye miradi ya barabara lengo likiwa ni kurahisisha usafiri kwa wananchi kwenda kwenye maeneo ya huduma za kijamii.


Kadhalika amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameendelea kuelekeza manunuzi yote ya Umma yapitie kwenye mfumo wa manunuzi wa kidigitali


Amesema mfumo huo unasaidia wazabuni kuingia kwenye mfumo ambao wenyewe unawachakata na kumpa zabuni mtu ambaye ana sifa zote za kupata ile za buni na ambaye hana sifa mfumo moja kwa moja unamtoa nje ya utaratibu.


" Ni mfumo ambao umeondoa malalamiko kwasababu kuna baadhi ya watu wamekuwa na malalamiko wanapewa zabuni wengine wao wanaachwa huku wakiwa na sifa  zinazotakiwa,".


"Watu wanakutana mezani wanamalizana kwenye meza pale wanapeana zabuni, lakini kupitia mfumo huu wa udhibiti wa manunuzi ya umma kwenye masuala ya zabuni sasa hakuna kukutana mezani ," ameaema.


Amesema lengo ni kudhibiti, kuhakikisha kwamba manunuzi ya Umma yote yanakwenda sawa sawa na jinsi ambayo ineelekezwa Ili kuhakikisha kwamba hakuna hujuma na ubadhilifu unaofanyika.


"Na tumefarijika kwamba ndugu zetu hawa wa TARURA wametumia mfumo huo vizuri na mradi umetekwlezwa kama ilivyolengwa" amesema.


Mradi huo wa Barabara ya mita 300 kuelekea Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha unaosimamiwa na Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) umejengwa kwa gharama ya sh.milion 495.8 fedha kutoka Serikali kuu na mpaka sasa sh. Miln 490,018,125 zimetumika.


Awali akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka Wilaya ya Bagamoyo , Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John amesema Mwenge huo utapita miradi 28 yenye thamani ya sh. Trillion 8.5 .


Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mwenge wa Uhuru umepitia katika mradi wa jengo la wagonjwa wa nje katika Zahanati ya Vikuruti, kituo cha wanafunzi wenye mahitaji maalumu shule ya Msingi Mlandizi, shughuli za mradi wa mapambano dhidi ya Malaria, shughuli za mapambano dhidi ya Ukimwi.


Miradi mingine ni kongani ya viwanda ya Sino Tan,  ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo shule ya Msingi Kilangalanga, shamba la mradi wa miti shule ya Sekondari Kawawa na mradi wa maji Kijiji Cha Ruvu stesheni ambao unasimamiwa na Mamlaka ya maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).



Matangazo

  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI WA BVR HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA January 23, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • MABADILIKO YA TAREHE YA USAILI September 24, 2024
  • Angalia Vyote

Matukio mapya

  • WWF YAKABIDHI MICHE YA MICHIKICHI KUHIFADHI KINGO ZA MTO RUVU

    May 24, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU NA UWEKAJI WAZI TAARIFA ZA MPIGA KURA AWAMU YA PILI YAFANYIKA KIBAHA

    May 14, 2025
  • WATAALAM WA AFYA PWANI WAKUTANA KUJADILI KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA WATOTO WACHANGA

    May 14, 2025
  • VIONGOZI WA VYAMA SIASA WARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA MKUU WA WILAYA NA MKURUGENZI MTENDAJI KIBAHA DC

    May 07, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Kuzindua bunge
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TOVUTI YA MKOA WA PWANI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA AJIRA
  • TOVUTI YA WANANCHI
  • TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI
  • TOVUTI YA WIZARA YA AFYA
  • TOVUTI YA EWURA

Tovuti Zinazoshabihiana

  • TAMISEMI
  • MKOA WA PWANI
  • TANZANIA
  • AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    KIBAHA DISTRICT COUNCIL

    Anwani ya Posta: P.O BOX 30153

    Simu ya Mezani: +255 23240224

    Simu: +255 0767520048

    Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM)
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.