• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kibaha District Council
Kibaha District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

  • Mwanzo
    • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • SP FINAL DRAFT
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasmali Watu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Usimamizi wa Sheria
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sehemu ya Mifugo
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uchumi na Mipango
      • Maadili
      • UKIMWI
      • Huduma za Jamii
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MAKALA MAALUM YA SIKU 365 ZA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Posted on: March 19th, 2022

MATOKEO YA SIKU 365 ZA SAMIA NADANI YA KIBAHA

KUELEKEA mwaka mmmoja wa uongozi wa Rais wa awamu ya sita  Samia Suluhu Hassan yapo mambo mengi yakujivunia katika Halmashauri ya Kibaha Vijijini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliingia madarakani baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tano John Pombe Magufuli aliyefariki Machi 17, 2021 na kifo chake kutangazwa na aliyekuwa Makamu wa Rais.

Rais Samia Suluhu Hassan kwa mujibu wa Katiba aliapishwa kuwa Rais wa  Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Machi 19 ,2021 ambapo alianza majukumu yake akiitangaza kauli mbiu yake ya "Kazi iendelee".

Kauli mbiu ya Rais Samia ilikua inamaanisha kuendeleza yale yaliyoanzishwa na Hayati John Pombe Magufuli hususani miradi mikubwa ya maendeleo ambayo ilianza kutekelezwa.

Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha ina miradi mingi ya kujivunia katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia .

“Kazi iendelee” imeendelea kwa kasi zaidi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kwa miradi ya maendeleo kwenye sekta mbalimbali zikiwemo  elimu na afya ambapo kiasi cha sh. billion 3.7 zimepokelewa na kutekeleza  miradi hiyo.

Siku 365 za Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya elimu amewezesha miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa thelathini (30) katika shule  za sekondari ambazo ni Rafsanjani Soga, Magindu ,Kwala Disunyara, Kawawa, Kilangalanga, Dosa Azizi na Mihande.

Aidha  Shule shikizi  Mkombozi na Mwembe Ngozi vyumba vya Madarasa ambavyo vimegharimu kiasi cha shilingi milioni mia sita(sh. 600,000,000), vilijengwa kwa Fedha ambazo zilitokana na mkopo wa masharti nafuu kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa UVIKO-19.

Katika kuendeleza kauli mbiu ya kazi iendelee Serikali ya awamu ya sita chini  ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa fedha za ujenzi wa vyumba vitano vya Madarasa  na matundu matano ya vyoo mbapo shule ya sekondari Disunyara imepokea shilingi  milioni mia moja( sh. 100,000,000/=) kwa ajili ya miradi hiyo.

"Shule hii ya Disunyara ni shule mpya iliyoanzishwa katika Kata ya Kilangalalanga ikiwa na lengo la kupunguza msongamano katika shule ya Kilangalanga hivyo madarasa haya matano yanakamilsha madarasa katika shule hiyo".

Kauli mbiu ya Kazi iendelee ya Rais Samia imeendelea kujidhihirisha kwa vitendo  kwani  hivi karibuni Halmashauri ya Wilaya ya kiibaha imepokea milioni mia moja na ishirini na tano (125,000,000) kwa ajili  ukamilishaji wa maboma ya shule za msingi. 

Kupitia kamati ya fedha na mipango ya Halmashauri hii walijadili  nakuona shule msingi Madege inauhitaji mkubwa wa madarasa hivyo walielekeza fedha zikajenge vyumba madarasa vitano kwenye shule hiyo.

Matunda ya siku 365 za Rais Samia yameendelea kuwaneemesha wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya kibaha kazi ambapo Serikali ilitoa pia milioni mia moja na ishirini na tano(125,000,000/=) kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba vya maabara katika shule za sekondari Mihande, Dosa azizi, Ruvustation, Kwala na Magindu.

Ujenzi wa vyumba hivi vya madarasa vimesaidia kupunguza changamoto za madarasa katika shule za sekondari na shule shikizi kwani  wapo wanafunzi walikuwa wanatembe umbali mrefu zaidi ya kilomita tano kufuata huduma ya elimu lakini kwa juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini uongozi makini wa rais Samia Suluhu Hassan changamoto hizo zimetatuliwa na watoto wanasoma kwa furaha na Amani kwenye majengo mazuri ya maradasa.

Kazi iliendelea vyema kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuunga mkono juhudi za wananchi ambao walianzishai ujenzi wa shule ya sekondari Kawawa baada ya kuona wanatembea umbali mrefu kuifuata shule wananchi waliamua kujenga madarasa matatu.

Kwa kuliona hilo Serikali ya wa awamu ya sita iliunga mkonoo juhudi hizo kwa kupeleka  kiasi cha fedha shilingi milioni thelathini na saba na laki tano (37,500,000/=) kwa ajili  ya kumalizia  vyumba hivyo vya madarasa.

Baadhi ya wazazi wameshukuru na kumpongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa zawadi hii yakudumu ya miundo mbinu ya elimu.

Kila mwananchi anatakiwa kuwa na afya nzuri ili aweze kufanya kazi kwa bidii na maarifa, kwa kulitambua hilo Mhe. Samia Suluhu Hassan ameipa kipaumbele sekta ya afya katika Halmashauri ya wilaya ya Kibaha kwa kutoa fedha kwa ajili ya kuendeleza  miradi ya afya.

Shilingi milioni mia tano zimepokelewa kwa ajili ujenzi wa wodi tatu (wodi ya watoto,wanaume na wanawake) katika hospitali ya wilaya iliyopo Disunyara Mlandizi, ujenzi wa wodi hizo upo katika hatua za ukamilishaji.

Pamoja na ujenzi wa wodi hizo Serikali imeleta fedha nyingine kiasi cha shilingi milioni mia nane kwa ajili kuendeleza ujenzi katika hospiotali ya Wilaya ambapo fedha hizo zitatumika kujenga chumba cha kuhifadhia maiti na wodi tatu za upasuaji .

Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha haikuwa na hospitali ya Wilaya tangu uhuru wa Tanganyika, serikali ya awamu ya tano chini uongozi wa Hayati John Pombe Magufuli ilitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya lakini haikukamilika na sasa kazi inaendelea chini ya uongozi wa awamu ya sita  mpaka sasa wodi ya baba, mama na mtoto zipo katika hatua ya ukamilishaji na wodi tatu za upasuaji zipo kwenye utekelezaji.

Kukamilika kwa hospitali hii ya wilaya kutakuwa msaada kwa wananchi wa Halmashauti ya Wilayani ya Kibaha, kwani wamekuwa wakifuata huduma za afya katika hospitali ya rufaa ya  Tumbi.

Pamoja ujenzi wa hospitali ya wilaya serikali ya awamu ya sita imetoa shilingi milioni mia moja ishirini na tano (tshs 125,000,000/=) kwa ajili ya ukamilishwaji wa zahanati tatu ambazo zimejengwa kwa nguvu za wananchi.

Serikali ya awamu ya sita pia iliweza kuwakumbuka watumishi na wananchi kwa kuboresha mazingira yao kazi na kutolea huduma kwa wananchi kwa kutoa  shilingi bilioni moja kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la Halmashauri lililopo Kisabi Mlandizi.

Kukamilika kwa jengo hilo kumeondoa kero ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma katika idara mbalimbali za Halmashauri hiyo ambapo kwa sasa wanazipata karibu na makazi yao.

Mwenyekiti wa Halmashauri .Erasto Makala amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweza kupambana na maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini ndani ya Wilaya ya Kibaha kwa kuweza kuboresha miundo mbinu ya afya na elimu.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha amempongeza Rais Samia Suluhu Hassani kwa anamna alivyofanikisha kuondoa vikwazo vya maendeleo katika Halmashauri hiyo.

Amesema kazi kubwa anayofanya Rais ni pamoja na kutoa fedha kwenye Halmashauri ambazo zinaenda kutekeleza miradi ya maendeleo yenye manufaa kwa wananchi.

" Katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita yapo mambo mengi ya maendeleo yamefanyika ikiwa ni pamoja na kupokea fedha sh. Miln 800 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la upasuaji  kwa wanaume, wanawake na jengo la upasuaji wa watu wote na jengo la kuhifadhia maiti ambayo yatajengwa katika hospitali ya wilaya " anaeleza.

Aidha anasema katika eneo la afya pia wamepokea kiasi cha sh. Miln 150 kwa ajili ya umaliziaji wa zahanati tatu ikiwemo ya Mpiji na Kipangege ambazo zilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi.

Anaeleza kuwa kwa upande wa mapato ya ndani wanatarajia kujenga zahanati mpya ya Vikuruti kwenye eneo ambalo lilikua halina huduma za afya karibu na wananchi.

Mkurugenzi ameipongeza awamu ya sita kwa mambo makubwa ambayo yamefanyika katika kipindi cha mwaka mmoja na kwamba wataendelea kusimamia fedha zinatolewa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo..

Mmoja wa wanafunzi katika shule ya sekondari Kawawa  Anna Haule ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuwajengea shule karibu na maeneo wanayoishi na kuondoa changamoto iliyokuwepo awali.

Anna anasema awali wanafunzi walikuwa wanalazimika kutembea km 20 kwa siku kwenda shule na kurudi nyumbani jambo ambalo lilisababisha baadhi yao kushindwa kumudu umbali huo na kukatisha masomo.

Anasema mbali ya umbali huo mrefu kwenda katika sekondari ya Disunyara pia kulikuwa na mlundikano wa wanafunzi uliokuwa unasababisha wengine kutoelewa kinachofundishwa na hivyo kufeli kwenye mitihani yao.

Jesca Isaya mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya Sekondari Disunyara amepongeza uongozi wa Rais Samia huku akisema kuwa kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Serikali ya awamu ya nne kimepunguza adha walizokuwa wanakabiliana nazo wanafunzi hususani katikq upande wa mlundikano.

Marehemu baba wa Taifa  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema kuna maadui watatu ambao ni ujinga,maradhi na umaskini ili tuweze kupambana na maadui hawa lazima tuhakikishe watu wetu wanapata elimu ambayo itakuwa ngao na ukombozi wa fikra , Rais kwa kutambua hayo amefanya mambo makubwa sana katika elimu.

 Maadui walioelezwa na  Mwalimu Nyerere sasa yanaonekana kuendelea kutekelezwa kwa vitendo na Rais Samia ambaye kwa mwaka mmoja amefanya maendeleo makubwa hali ambayo inaashiria kuwa na mabadiliko makubwa katika kipindi cha uongozi wake.


Matangazo

  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI WA BVR HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA January 23, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • MABADILIKO YA TAREHE YA USAILI September 24, 2024
  • Angalia Vyote

Matukio mapya

  • KAIMU KATIBU TAWALA WILAYA YA KIBAHA ATOA WITO KWA WENYEVITI WA MJI MDOGO MLANDIZI KUZINGATIA UADILIFU

    February 11, 2025
  • MAKAMU WA RAIS AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, ATOA WITO DHIDI YA UBADHILIFU

    April 02, 2025
  • ELIMU YA LISHE JUU YA USINDIKAJI WA BIDHAA ZA VYAKULA YATOLEWA KIBAHA DC.

    March 23, 2025
  • Mwenyekiti wa Halmashauri Amshukuru Rais Samia kwa Fedha za Miradi

    February 05, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Kuzindua bunge
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TOVUTI YA MKOA WA PWANI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA AJIRA
  • TOVUTI YA WANANCHI
  • TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI
  • TOVUTI YA WIZARA YA AFYA
  • TOVUTI YA EWURA

Tovuti Zinazoshabihiana

  • TAMISEMI
  • MKOA WA PWANI
  • TANZANIA
  • AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    KIBAHA DISTRICT COUNCIL

    Anwani ya Posta: P.O BOX 30153

    Simu ya Mezani: +255 23240224

    Simu: +255 0767520048

    Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM)
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.