Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini Erasto Makala ametoa wito kwa kaya masikini zitakazoingia kwenye utekelezaji wa sehemu ya pili ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) awamu ya tatu kuhakikisha wanaibua miradi ya miundombinu.
Makala alitoa wito huo jana wakati wa kikao cha siku moja cha kujenga uelewa kuhusu kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF na kutoa muongozo wa utambuzi na uandikishaji wa kaya za walengwa katika eneo la utekelezaji kilichofanyika Mlandizi na kuwashirikisha Madiwani, wakuu wa idara na wawezeshaji.
Mwenyekiti huyo alisema katika awamu iliyopita ya utekelezaji wa TASAF ipo miradi ilitekelezwa ikiwemo mradi wa lambo la maji Lukenge na Magondu ambayo imekuwa imeondoa kero iliyokuwepo awali.
Alisema kaya zitakazoingia kwenye mpango katika awamu hii zinatakiwa kuibua ubovu wa miundombinu katika maeneo yao hususani barabara.
"Nawashukuru TASAF kwa lengo lao la kunusuru kaya masikini, nawaomba katika awamu hii pia wajikite miundombinu ya vyumba vya madarasa naamini wataendelea kufanya mambo.makubwa kuliko awali, na kaya za walengwa zitafanya kazi kwa bidii kujiongezea kipato" alisema Makala.
Naye Diwani wa viti maalumu Josephine Gunda alisema kaya zilizonufaika katika awamu iliyopita zimekuwa na mabadiliko kiuchumi ambapo aliomba idadi ya kaya za wanufaika iongezwe kwani walioachwa awali walikua wengi.
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Afisa kutoka katika Mfuko huo Zuhura Mdungi alisema utekelezaji wa moango wa kunusuru kaya masikini pia umewezesha kaya za walengwa kujikita kwenye shughuli za kukuza kipato na kujiimarisha kiuchumi ikiwemo ufugaji, uvuvi, Kilimo na biashara.
Zuhura alisema katika kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF kitafikia zaidi ya kaya milion 1450,000 zenye watu zaidi ya milion saba kote nchini ikiwa ni nyongeza ya kaya 350,000.
Alisema mpango huo utawezesha kaya masikini zinazoishi katika hali duni hususani watoto na akina mama wajawazito kupata lishe bora, husuma za afya na Elimu.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.