Wajumbe wa kamati ya lishe wamekutana katika kikao cha kujadili taarifa ya utekelezaji wa Mkataba wa lishe kwa robo ya kwanza 2023/2024.
Akizungumza kwenye kikao hicho Kaimu afisa lishe wilaya Bonza Mshana amesema suala la lishe ni mtambuka hivyo linapewa kipaumbele ili kuhakikisha wananchi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wanafikiwa na kupatiwa elimu sahihi ya masuala ya lishe ili kuepukana na utapiamlo .
Aidha Bonza amesema katika robo ya kwanza waliadhimisha wiki ya unyonyeshaji ambapo jumla ya wazazi/ walezi 2897 walipatiwa unasihi wa unyonyeshaji maziwa ya mama pekee kwa watoto wachanga hadi kufikia miezi 6 na kuendelea kuwapa vyakula limbikizi pamoja na kuwanyonyesha watoto hadi kufikia miaka miwili kupitia vituo vya kutolea huduma za afya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Butamo Ndalahwa alisema kwa mwaka 2022/2023 Halmashauri ilishika nafasi ya kumi kitaifa katika Utekelezaji wa mkataba wa ya lishe na kumpongeza Kaimu afisa lishe kwa juhudi za kuboresha swala la lishe.
Aidha ili kuhakisha wanafunzi wanakula vyakula vilivyoongezewa virutubishi Butamo alitoa agizo kwa idara ya manunuzi kuhakikisha wazabuni wote wanaopewa kazi ya kusambaza vyakula shuleni kama unga wa mahindi uwe umeongezewa virutubishi.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.