Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, leo tarehe 31.10.2023, wamefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kwa robo ya kwanza 2023/2024.
Miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ni pamoja na Bustani ya Wanyama (zoo) ya Ruvu JKT ambapo wameweza kujionea maandalizi ya uazishwaji wa Bustani ya Wanyama.
Pi, Kamati hiyo imeweza kujionea ufugaji wa samaki wa Sato kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Vilevile Kamati hiyo iliwatembelea walengwa wa TASAF waliopata ruzuku za uzalishaji kupitia mpango wa kuweka akiba na kukuza uchumi wa kaya.
Wakizungumza na wajumbe wa kamati hiyo, wanufaika hao walithibitisha kupata mafunzo ya ujasiriamali kabla ya kupokea fedha hizo kwa ajili ya uboreshaji wa shughuli zao za kuongeza kipato.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Paul aliwashauri walengwa waliopata ruzuku kutumia fedha walizopata vizuri kulingana na mipango ya biashara zao kwani wanaandaliwa kuhitimu kwenye mpango.
Kamati ilitembelea Kikundi kingine cha Wanawake na Maendeleo Kata ya Mtongani kinachojishughulisha na uuzaji wa nafaka.
Kikundi hiki ni mojawapo ya vikundi vya wanawake vinavyonufaika na mkopo wa asilimia kumi kutoka Halmashauri. Wajumbe wa Kamati wamekipongeza kikundi hiki kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana ikiwamo kurejesha mkopo wa milioni 15 kwa wakati na bado biashara ya kuuza nafaka inaendelea vizuri.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.