• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kibaha District Council
Kibaha District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

  • Mwanzo
    • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • SP FINAL DRAFT
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasmali Watu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Usimamizi wa Sheria
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sehemu ya Mifugo
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uchumi na Mipango
      • Maadili
      • UKIMWI
      • Huduma za Jamii
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Yavuka Malengo ya Ukusanyaji mapato

Posted on: November 23rd, 2023

Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani imevuka lengo la ukusanyaji wa mapato kwa asilimia 14 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024.


Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Erasto Makala amesema kwa robo ya kwanza ya Mwezi Julai hadi September wameweza kukusanya mapato kwa asilimia 39.


Makala amebainisha hayo katika kikao cha Baraza la Madiwani  kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri  hiyo na kuhudhuriwa na wataalam na watendaji kutoka katika ngazi mbalimbali.


Hali kadhalika, Makala ametaka fedha hizo zitumike kama ilivyopangwa, yaani asilimia 40 ya mapato hayo yaende kwenye miradi ya maendeleo na asilimia 60 iende kwenye matumizi ya kawaida.


Amesema  miradi ya maendeleo itakayotekelezwa na mapato hayo ni miradi ya afya, elimu na barabara kwani bajeti ya TARURA ni finyu na haikidhi mahitaji ya wananchi; hivyo Halmashauri itatekeleza miradi mingine ya barabara.


Vilevile, ameeleza kwamba wataangalia vipaumbele vya wananchi kwa kwenda kuwaongezea nguvu kwenye miradi walioanzisha na haikukamilika.

Akizungumza katika Kikao hicho Diwani wa Kawawa, Mhe. Alfred Malega, ameitaka Halmashauri kwenda kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kupitia fedha za mapato ya ndani ikiwemo kufungua barabara ambazo hazipitiki kwa sasa kutokana na mvua.


Malega amesema Kibaha vijijini inaenda kubadilika kutokana na uwekezaji mkubwa wa viwanda uliofanyika; hivyo Halmashauri  inatakiwa kuweka miundombinu vizuri.


Naye Gloria Mshindo, Diwani wa Viti Maalum amesema kuongezeka kwa mapato ni neema kwa wananchi wa Halmashauri hii kwani huduma za afya zinaenda kuboreshwa.


Awali, Mbunge wa Kibaha Vijijini, Michael Mwakamo alisema kwa mwaka wa fedha 2023/2024, vipaumbele kwenye fedha za Mfuko wa Jimbo ni ukamilishaji wa ofisi za vitongoji pamoja na  miradi ya Elimu na afya ambayo haijakamilika


Mwakamo amewataka Madiwani ambao wana mahitaji nje ya vipaumbele alivyovitaja, wasilete maombi kwa mwaka huu mpaka miradi iliyopo ikamilike.

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI WA BVR HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA January 23, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • MABADILIKO YA TAREHE YA USAILI September 24, 2024
  • Angalia Vyote

Matukio mapya

  • WWF YAKABIDHI MICHE YA MICHIKICHI KUHIFADHI KINGO ZA MTO RUVU

    May 24, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU NA UWEKAJI WAZI TAARIFA ZA MPIGA KURA AWAMU YA PILI YAFANYIKA KIBAHA

    May 14, 2025
  • WATAALAM WA AFYA PWANI WAKUTANA KUJADILI KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA WATOTO WACHANGA

    May 14, 2025
  • VIONGOZI WA VYAMA SIASA WARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA MKUU WA WILAYA NA MKURUGENZI MTENDAJI KIBAHA DC

    May 07, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Kuzindua bunge
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TOVUTI YA MKOA WA PWANI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA AJIRA
  • TOVUTI YA WANANCHI
  • TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI
  • TOVUTI YA WIZARA YA AFYA
  • TOVUTI YA EWURA

Tovuti Zinazoshabihiana

  • TAMISEMI
  • MKOA WA PWANI
  • TANZANIA
  • AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    KIBAHA DISTRICT COUNCIL

    Anwani ya Posta: P.O BOX 30153

    Simu ya Mezani: +255 23240224

    Simu: +255 0767520048

    Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM)
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.