Kukamilika kwa ujenzi wa vyumba 30 vya madarasa kwa shule za msingi na Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani kutawezesha uwepo wa ongezeko la wanafunzi kutoka 7,275 hadi kufikia 8690 hali inayoelezwa kuwa ni njia moja wapo ya kuinua kiwango cha Elimu kwa jamii.
Kabla ya ujenzi huo Halamashauri hiyo imekuwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa 7 hali ambayo imekuwa ikisababisha wanafunzi kusoma wakiwa wamelundikana kwa chumba kimoja zaidi ya 50 hivyo kushindwa kusoma kwa nafasi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Afisa Elimu Halmashauri hiyo aliyoisoma kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Sara Msafiri jana alisema kuwa ujenzi wa madarasa hayo umetokana na pesa za uvico na kwamba mpaka sasa wameshakamilisha ujenzi kwa asilimia 100.
Alisema kuwa Halmashauri hiyo ilipokea sh. m. 600 kwaajili ya ujenzi wa vyumba 30 vya madarasa ambapo kati ya hivyo 20 vya shule ya sekondari na 10 ni upande wa shule za msingi.
Alisema kuwa katika ujenzi huo pia wamefanikiwa kujenga shule mpya ambazo zitawezesha kupokea wanafunzi wa sekondari wa kidato cha kwanza na wale wa vidato vingine ambao awali walikuwa walikuwa wanalazimika kutembea umbali wa km 10 kwa siku kufuata masomo kutokana umbali wa makazi na maeneo ya shule.
"Mpaka sasa tumeshakamilisha hatua zote na tuna uhakika kuwa jumatatu ya january 17 wanafunzi wote wataanza masomo na hatutakuwa na awamu mbili za kuwapangia shule wanafunzi wote waliofaulu"alisema.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Michael Mwakamo aliwataka walimu na wanafunzi watakaoyatumia madawati pamoja na madarasa hayo kuyatunza ili yatumike kwa vizazi vilivyopo na vile vijavyo.
"Akizungumza baada ya kupokea vyumba hivyo vya madarasa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Sara Msafiri alisema kuwa wanafunzi wa shule za sekondari na msingi Wilayani huko watakaobainika kuvunja madawati kwa makusudi wazazi wao wataajibika kulipa ili kulipa mafundi watakaotengeneza.
Alisema kuwa kutokana n juhudi zilizofanywa naSerikali kukopa pesa na kughalimia ujenzi huo halipaswi kuweka mchezo na kuwafumbia macho watu wachache watakaoonekana kurudisha nyuma jitihada hizo.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.