Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Sara Msafiri amewataka watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kufanya kazi kwa kushirikiana na kusaidiana ili kazi katika idara ziweze kufanyika kwa ufanisi.
Dc Msafiri ameyasema hayo alipofanya kikao na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya kibaha siku ya ijumaa kwenye makao makuu ya halmashauri hiyo yaliyopo Mlandizi Kisabi.
Akiongea wakati wa kikao hicho Msafiri alisema lengo la kikao hicho ni kujitambulisha kwa watumishi wa Halmshauri hiyo, sambamba na kujitambulisha Msafiri aliwataka watumishi kuendeleza utaratibu wa nidhamu kazini uliowekwa na awamu ya tano ,kwani kuna badhii ya watumishi wameanza kufanya kazi kwa kulegalega.
Msafiri pia aliwataka watumishi watende haki kwa wananchi wanaowahudumia kwani serikali ya awamu ya sita imejielekeza kwenye kutenda haki.
Pamoja na hayo Dc aliwataka wakuu wa idara kusimamia kwa umakini miradi inayoletwa kwenye Halmashauri na kuzingatia ubora wa miradi hiyo,pamoja na kuhakikisha certificate kwa ajili ya malipo zinatolewa kwa wakati na kufuatiliwa kwa ukaribu.
Dc aliwahakikishia watumishi kuwa barabara inayoelekea kwaenye jengo la halmashauri itatengenezwa hivyo watumishi wasiwe na hofu.
Akiongea wakati wakufungua kikao hicho Mkurugunzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Butamo Ndalahwa alimpongeza Dc kwa kuaminiwa tena na Mhe. Rais na kumhakikishia kuwa wako tayari kufanya nae kazi kwa ushirikiano na watakapokosea wapo tayari kukosolewa.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.