Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege amezindua madarasa 32 na ofisi nne za walimu katika shule za sekondari,yaliyojengwa kupitia kampeni ya ELIMISHA KIBAHA,mkoani Pwani ambayo yatapunguza changamoto iliyokuwepo awali ya mlundikano wa wanafunzi madarasani na yatatumiwa na wanafunzi takriban 900.
Katika hafla hiyo ya kukabidhi madarasa hayo,amewaasa wazazi na walezi kuwapa elimu watoto wao na kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya taaluma zao ili baadae watumie fursa ya viwanda vinavyojengwa kwa wingi mkoani humo .
Alisema ELIMISHA KIBAHA ni kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuhakikisha elimu inatolewa bure kwa kila mwanafunzi wa darasa la awali hadi kidato cha nne.
“Haya ni maelekezo ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015,ambayo nina ujasiri wa kusema ninyi Kibaha, mmetekeleza,na nawaagiza wakuu wa wilaya wengine waige mfano wako mkuu wa wilaya ya Kibaha ambae umebuni kampeni hii na kuzaa matunda”alisema Kandege.
Alieleza, hii ni hatua kubwa ,kwani kama mkuu huyo wa wilaya angekaa kusubiri ruzuku ya serikali kuu ama mapato ya halmashauri ndiyo yajenge azma hii isingetimia kwa mwaka mmoja huu.
Kandege alifafanua ,kiuhalisia haiwezekani kuwa na Taifa lililoelimika kama hakuna mazingira bora ya sekta ya elimu ,hali itakayofanya watanzania wawe na ujuzi wa kutosha katika matumizi ya rasilimali zilizopo na fikra chanya za maendeleo. Hivyo,ubunifu uliofanyika umelenga katika kufikia malengo ya dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.
‘”Mkoa wa Pwani umejikita katika uwekeaji wa viwanda ambapo kuna viwanda 47 ambavyo ni vikubwa,vya kati na vidogo vinavyofanyakazi,hii ni fursa kwa wanafunzi kuchangamkia ,kwani bila vijana wetu kuwa na elimu nafasi za kazi za kitaalamu kwenye viwanda hivyo vitachukuliwa na vijana wa mikoa mingine na nje ya nchi.”alisema Kandege.
Nae Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Mhe.Assumpter Mshama amesema chimbuko la kampeni ya elimisha Kibaha limetokana na upungufu wa madarasa uliojitokeza mwaka 2019 kutokana na kuongezeka kwa ufaulu mwaka 2018 hali iliyosababisha baadhi ya shule wanafunzi waingie kwa awamu mbili.
“Kufuatia hali hii nilishirikiana na wadau wa maendendeleo ili kuondoa upungufu wa madarasa uliopo kwa halmashauri ya wilaya madarasa 34 na halmashauri ya Mji
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.