• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kibaha District Council
Kibaha District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

  • Mwanzo
    • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • SP FINAL DRAFT
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasmali Watu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Usimamizi wa Sheria
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sehemu ya Mifugo
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uchumi na Mipango
      • Maadili
      • UKIMWI
      • Huduma za Jamii
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Zahanati ya Mpiji Yafunguliwa Rasmi

Posted on: November 1st, 2022

Wananchi wa Kijiji cha Mpiji kata ya Bokomnemela, Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani wamefurahia  ufunguzi wa Zahanati ya Kijiji hicho ambacho walianza ujenzi kwa nguvu zao hadi kufikia hatua ya boma ndipo Serikali Kuu ikawapatia  Shilingi milioni 50  na  Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha ikawaongezea milioni 17 kutoka mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa vyoo.

Wakiongea katika Siku ya Afya ya Kijiji na Ufunguzi wa Zahanati hiyo, wananchi wa Kijiji cha Mpiji Station wameishukuru Serikali na viongozi mbalimbali kwa kufanikisha umaliziaji wa zahanati yao ambayo itakuwa mkombozi kwao kwani walikuwa wanatembea umbali mrefu kufuata huduma za afya huku mama wajawazito wakijifungulia njiani.

Vilevile, Mganga Mkuu wa halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Dkt Wilfred Kondo, amesema wamepokea watumishi wawili kutoka TAMISEMI ambao wamepangwa katika zahanati hiyo; hivyo basi, zahanati itaanza kutoa huduma za wagonjwa wa nje, mama wajawazito na huduma za maabara.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa zahanati hiyo, Diwani wa Kata ya Bokomnemela, Paul Boniphace Maguhwa amesema Kijiji cha Mpiji Station kilikuwa na changamoto kubwa sana ya zahanati kwani waliwahi kushuhudia mama mjamzito akijifungulia mtoni kutokana na jiografia ya kijiji chao kutenganishwa na mto kwenda kijiji kingine. Kipindi cha mvua wananchi walikuwa wakipata shida sana.

Kutokana na changamoto hizo, waliamua kuanzisha ujenzi wa zahanati kwa kutumia nguvu zao hadi walipofikia hatua ya boma ambapo Serikali iliwasaidia kumalizia. Aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwajali wananchi wa hali ya chini.

Mwenyekiti wa Huduma za Jamii wa Halamshauri ya Wilaya ya Kibaha, Shomari Minshehe,   alisema kuwa Halmashauri ina mpango wa kusogeza huduma za afya kwa wanananchi; hivyo basi, ilibaini maeneo yote yenye changamoto za huduma ya afya mojawapo ni Kijiji cha Mpiji  na kuamua kupeleka fedha za kumalizia jengo ambalo lilianza kujengwa  kwa nguvu za wanannchi na kulikamilisha.

Minshehe alisema kuwa Halmashauri ina mpango wa kila kijiji kuwa na zahanati ili kuwaondolea wananchi kero ya kufuata huduma za afya mbali.

Aidha, mwenyekiti huyo aliwataka wananchi kuanzisha ujenzi wa nyumba za watumishi na Serikali itawaunga mkono ili watumishi hao wakae karibu na zahanati.

Shabani Kamunya, mwananchi wa Kijiji cha Mpiji Station amesema tangu uhuru wananchi wamekuwa wakipata changamoto kubwa sana ya afya. Wajawazito wengi wamejifungulia njiani kwani kijiji chao kipo pembezoni mwa wilaya, ndiyo maana waliamua kwa nguvu zao kuanza ujenzi wa zahanati yao hadi kufikia hatua ya boma bila malumbano. Pia, ameishukuru Serikali kwa kumaliza ujenzi wa zahanati yao na kuwaletea watumishi.

Saphia Seifu, Mwananchi wa Kijiji cha Mpiji Station amemshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwaonea huruma wanawake wenzake kupata zahanati kwani walikuwa wanapata adha sana ya huduma za afya.

Zahanati ya Mpiji Station imejengwa kwa nguvu za wananchi na kumaliziwa na fedha kutoka Serikali Kuu na Halmashauri. Zahanati imeanza kutoa huduma mbalimbali ikiwamo huduma za mama wajawazito kujifungua na huduma za maabara ambapo katika ufunguzi wananchi wamepewa huduma mbalimbali za afya  bure zikiwamo vipimo, chanjo  na ushauri wa lishe kwa wamama wajawazito na watoto huku wananchi wengine wakichangia damu.

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI WA BVR HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA January 23, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • MABADILIKO YA TAREHE YA USAILI September 24, 2024
  • Angalia Vyote

Matukio mapya

  • KAIMU KATIBU TAWALA WILAYA YA KIBAHA ATOA WITO KWA WENYEVITI WA MJI MDOGO MLANDIZI KUZINGATIA UADILIFU

    February 11, 2025
  • MAKAMU WA RAIS AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, ATOA WITO DHIDI YA UBADHILIFU

    April 02, 2025
  • ELIMU YA LISHE JUU YA USINDIKAJI WA BIDHAA ZA VYAKULA YATOLEWA KIBAHA DC.

    March 23, 2025
  • Mwenyekiti wa Halmashauri Amshukuru Rais Samia kwa Fedha za Miradi

    February 05, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Kuzindua bunge
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TOVUTI YA MKOA WA PWANI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA AJIRA
  • TOVUTI YA WANANCHI
  • TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI
  • TOVUTI YA WIZARA YA AFYA
  • TOVUTI YA EWURA

Tovuti Zinazoshabihiana

  • TAMISEMI
  • MKOA WA PWANI
  • TANZANIA
  • AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    KIBAHA DISTRICT COUNCIL

    Anwani ya Posta: P.O BOX 30153

    Simu ya Mezani: +255 23240224

    Simu: +255 0767520048

    Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM)
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.