• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kibaha District Council
Kibaha District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

  • Mwanzo
    • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • SP FINAL DRAFT
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasmali Watu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Usimamizi wa Sheria
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sehemu ya Mifugo
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uchumi na Mipango
      • Maadili
      • UKIMWI
      • Huduma za Jamii
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Wiki ya Uwekezaji na Biashara Pwani

Posted on: October 6th, 2022


RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete amewaasa wenye viwanda Mkoani Pwani na nchi kijumla kuzalisha bidhaa bora zinazolingana na soko la ushindani katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kujiinua kimasoko.


Aidha ameutaka mkoa huo kuboresha Mazingira ya Uwekezaji na kusimamia maeneo yanayotengwa kwa ajili ya uwekezaji (kongani) kwa kuzingatia maendeleo yanavyokuwa kwa maslahi ya vizazi vijavyo.


Akifungua maonyesho ya tatu ya wiki ya biashara na uwekezaji Mkoani Pwani yanayofanyika Mailmoja Kibaha Mjini,Kikwete alieleza Tanzania ni miongoni mwa nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki ambapo zipo nchi saba hivyo Kuna kila sababu ya kuzalisha bidhaa zenye viwango na ubora .


"Hatua tuliyofikia tupo katika ushindani Lazima tuzalishe bidhaa zetu na kuwa bora ,nchi yetu imesaini Africa Continental free trade area ,biashara huru Afrika ,mtakuja kusema Serikali izue bidhaa zinazojiuza Lakini tutashindwa kwakuwa mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki itafungua "


"Tuhakikishe tunazalisha bidhaa Bora vinginevyo itakula kwetu,hata kama tunazalisha kibongobonho lakini hao wabongo wanataka bidhaa bora pia"alisisitiza Kikwete.


Hata hivyo Kikwete alisema ,Uchumi unakuwa kwa uwekezaji Kama hakuna uwekezaji hakuna uchumi na utakwama na kusinyaa.


Alibainisha kwamba ,kihistoria mkoa umekuwa kwa kivuli Cha Dar es Salaam kwa mambo mbalimbali wakati huo mkoa wa Pwani ukijumlishwa na Dar es Salaam, Sasa ni wakati wa mkoa wa Pwani kutumia fursa hiyo.


"Mungu bariki Dar es salaam imejaa Sasa ni wakati wetu sisi mkoa wa Pwani ,ndio ukweli wa historia anayetaka aje kuwekeza ,atakaetaka kuwekeza Dar es Salaam labda kujenga kwenye maghorofa."


Vilevile aliwashauri kusimamia Maeneo wanayojenga viwanda ,kwani vipo viwanda vilivyojengwa wilayani Mkuranga ambavyo vipo barabarani kulingana na mahitaji na maendeleo yanavyokuwa vinaweza kuja kumegwa kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara.


Kikwete alimpongeza mkuu wa mkoa wa Pwani alhaj Abubakari Kunenge kwa kutenga maeneo ya uwekezaji,kongani za viwanda.


"Katika hili niliuliza pale Katika Banda la wafadhili wakuu wa maonyesho haya SINOTAN Kuwa wamepewa eneo la hekari 2,500 , watajenga viwanda 400 na kutoa ajira ya watu laki moja Sasa wataishi wapii,nimejibiwa Kuna Mazingira mazuri tayari kunapimwa maeneo ya watu kujenga ,


"Msije kupima maeneo kwa gharama kubwa ambayo watu wa uwezo wa chini hawatamudu ,wekeni gharama nafuu na nashukuru pale kwangu nipo na Naibu Waziri wetu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi nitamwambia yasiwe maeneo watakayomudu matajiri Ila na wengine wa Hali ya chini "alishauri Kikwete.

Katika hatua nyingine Kikwete alisema Serikali inafanya kazi nzuri,katika kuinua sekta ya uwekezaji na viwanda na kuimarisha Mazingira bora ya uwekezaji.

"Tumeona Mamlaka ya maji safi na maji taka (DAWASA) wanavyoweka nguvu kubwa ya kuboresha miundombinu ya maji safi na salama na kufikisha kwenye maeneo ya uwekezaji , Serikali imejenga reli ya kisasa (SGR), imeongeza huduma za usafiri wa anga na vingine vimejengwa na kujenga kongani za viwanda."


Alisema uwekezaji una manufaa makubwa katika kutoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja ,ambapo itasaidia vijana kupata ajira na kuondokana na kushinda kucheza pool.

MKURUGENZI WA SINOTAN

Mkurugenzi wa SINOTAN Jensen Huang alisema wanaendelea na michakato mbalimbali ambapo wamelenga kujenga viwanda 400 na wamepata hekari zipatazo 2,500.

Alisema wanatarajia kutoa ajira kwa watu zaidi ya laki moja na wanaahidi kuwapa kipaombele wazawa.

Jensen alieleza hadi kufikia Juni 2023 watakuwa wamejenga viwanda kumi kati ya malengo waliyojiwekea.


MKUU WA MKOA PWANI

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Pwani alhaj Abubakari Kunenge alieleza mkoa una viwanda 1,460 kati ya hivyo 90 ni vikubwa.


Alieleza kwamba ,mkoa huo imejipanga katika sera ya uwekezaji na viwanda kwa kutekeleza kwa vitendo .


"Ukitaka kuwekeza njoo Mkoani Pwani,tumejipanga kwa kuweka Mazingira Bora na ulinzi na Usalama ,tumeboresha miundombinu ya barabara,maji,umeme kwa ajili ya viwanda"


"Pia kwa kuzingatia masuala ya uwekezaji na changamoto zao mkoa tumetenga kila siku ya Jumanne tuna Taasisi 19 ambazo zinasikiliza kero za wawekezaji na kuzitafutia ufumbuzi"alisema Kunenge.


Kunenge alielezea Kuwa ,katika uwekezaji wamesheheni kwenye nyanja zote ikiwemo kilimo, biashara, ufugaji,uchumi wa blue (utalii) Kuna fukwe yenye km.1,132 kwa ajili ya uwekezaji,Kuna saadan, selou iliyopo Rufiji ambapo mkoa una jumlanya vivutio 72.


Akifafanua zaidi Kunenge alisema ,upande wa maji kwa wawekezaji na kusambaza maji kwa jamii RUWASA na DAWASA mkoa zinafikisha maji kwa asilimia 86.


Anasema Serikali ilipeleka Bilioni 197 kwa Ruwasa na DAWASA  kwa ajili ya kuhakikisha inasogeza huduma ya maji ndani ya mkoa na hatua mbalimbali za zinaendelea huku miradi mingine ikiwa imekamilishwa.


MKURUGENZI SIDO


Katika maonyesho hayo Mkurugenzi  Mkuu SIDO  Pro. Silvester Mpanduji  alisema lengo la Sido kushiriki maonyesho ni kuunganisha wafanyabiashara ,kuinua masoko na kutafuta fursa mbalimbali za biashara.


Sambamba na hayo alisema mwaka 2021 Serikali ilitoa sh. Bilion 3.1 kwa mfuko wao wa maendeleo ambapo vituo vya teknolijia saba vimejengwa ikiwemo Tanga, Singida na Geita .


Pia Shirika hilo limetoa mikopo kwa watu zaidi ya 2,694 kwa kiasi cha sh.bilion 6.4 fedha kutoka moja kwa moja Sido na kwamba wamewezesha viwanda 247 katika kipindi cha mwaka 2021 na kwamba wametoa mafunzo kwa wajasiriamali 19,000 .



Pro.Mpanduji alisema wanakabiliwa na vikwazo katika maeneo ya kufanyia kazi pamoja na elimu ya biashara kwa wajasiriamali hivyo wanahitaji fedha zaidi kukidhi mahitaji ya wafanyabiashara.


Alitoa rai kwa Watanzania kupenda na kuvienzi viwanda vidogo vidogo lakini pia kununua bidhaa zinazozalishwa katika viwanda hivyo ili kuviwezesha viweze kupiga hatua zaidi.


Maonyesho ya tatu ya wiki ya biashara na uwekezaji Mkoani Pwani,yalianza mwaka 2018 akiwa mkuu wa mkoa wakati huo Evarist Ndikilo ,na haya ya Sasa ni Mara ya tatu ambapo yameandaliwa na mkoa kwa kushirikiana na SIDO ,kuratibiwa na Tantrade na wafadhili wakuu ni SINOTAN.




Matangazo

  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI WA BVR HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA January 23, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • MABADILIKO YA TAREHE YA USAILI September 24, 2024
  • Angalia Vyote

Matukio mapya

  • KAIMU KATIBU TAWALA WILAYA YA KIBAHA ATOA WITO KWA WENYEVITI WA MJI MDOGO MLANDIZI KUZINGATIA UADILIFU

    February 11, 2025
  • MAKAMU WA RAIS AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, ATOA WITO DHIDI YA UBADHILIFU

    April 02, 2025
  • ELIMU YA LISHE JUU YA USINDIKAJI WA BIDHAA ZA VYAKULA YATOLEWA KIBAHA DC.

    March 23, 2025
  • Mwenyekiti wa Halmashauri Amshukuru Rais Samia kwa Fedha za Miradi

    February 05, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Kuzindua bunge
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TOVUTI YA MKOA WA PWANI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA AJIRA
  • TOVUTI YA WANANCHI
  • TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI
  • TOVUTI YA WIZARA YA AFYA
  • TOVUTI YA EWURA

Tovuti Zinazoshabihiana

  • TAMISEMI
  • MKOA WA PWANI
  • TANZANIA
  • AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    KIBAHA DISTRICT COUNCIL

    Anwani ya Posta: P.O BOX 30153

    Simu ya Mezani: +255 23240224

    Simu: +255 0767520048

    Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM)
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.