• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kibaha District Council
Kibaha District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

  • Mwanzo
    • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • SP FINAL DRAFT
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasmali Watu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Usimamizi wa Sheria
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sehemu ya Mifugo
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uchumi na Mipango
      • Maadili
      • UKIMWI
      • Huduma za Jamii
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

WENYEVITI MAMLAKA YA MJI MDOGO MLANDIZI WAHIMIZWA KUPELEKA MAENDELEO KWA WANANCHI NA KULINDA MIPAKA YA VITONGOJI

Posted on: June 5th, 2025



Baraza la robo ya tatu la Mamlaka ya Mji Mdogo Mlandizi kwa mwaka wa fedha 2024/2025 limefanyika leo Juni 5, 2025, katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, ambapo wajumbe walijadili utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kupata elimu kuhusu uendeshaji wa mamlaka hiyo.


Katika barazs  hilo, Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Edward Masona, alitoa elimu kwa wajumbe kuhusu taratibu za uendeshaji wa mamlaka ya mji na mchakato wa kuifikisha Mlandizi kuwa Halmashauri ya Mji.

 Elimu hiyo ilitolewa kufuatia maswali kutoka kwa wajumbe waliotaka kujua hatua za kufuata kufanikisha azma hiyo.


Akizungumza kwenye baraza hilo  Katibu wa Chama cha mapinduzi (CCM)  Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha ,Ole  Ezekiel Mollel aliwataka wenyeviti wa Mamlaka ya Mji Mdogo Mlandizi kuhakikisha wanawapelekea wananchi maendeleo kama walivyoaminiwa na chama hicho.

“Chama kimewaamini. Pelekeni maendeleo kwa wananchi. Jukumu lenu ni kushirikiana na watendaji wa serikali kuleta maendeleo, hasa kipindi hiki serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan inaleta fedha nyingi sana za miradi,” alisema Ole.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Bi. Regina Bieda, aliwahimiza wenyeviti hao kufanya kazi kwa kujiamini kwani wamechaguliwa na wananchi kwa imani kuwa wataweza kutatua changamoto zilizopo.

“Wenyeviti mmekuwa chombo muhimu kwenye vitongoji vyenu. Ninyi ndio wakurugenzi, Ma DC, maafisa ustawi wa jamii na wengineo. Pokeeni wananchi, wasaidieni na waelekezeni sehemu sahihi za kupeleka changamoto zao,” alisema Bi. Bieda.


Aidha, aliwataka kulinda mipaka ya vitongoji vyao ili visivamiwe na wilaya nyingine, kuimarisha usafi ndani ya mji mdogo wa Mlandizi na kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa ajili ya kuharakisha maendeleo.


Katika kikao hicho, katibu Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)Godfrey Dzombe  aliwasisitiza viongozi hao kuboresha mahusiano na watendaji wa serikali, akieleza kuwa mahusiano mazuri ni njia muhimu katika kufanikisha maendeleo

Matangazo

  • FURSA ZA AJIRA ZA MUDA KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU 2025 July 05, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • MABADILIKO YA TAREHE YA USAILI September 24, 2024
  • Angalia Vyote

Matukio mapya

  • JUKWAA LA WANAWAKE KIBAHA DC LAFANYA UCHAGUZI, DKT. MAIMUNA AIBUKA MWENYEKIT

    June 23, 2025
  • MADIWANI KIBAHA WAAGWA RASMI, MAFANIKIO YASISITIZWA KAMA URITHI WA USHIRIKIANO

    June 20, 2025
  • HALMASHAURI YA KIBAHA YAZINDUA ZOEZI LA UNYUNYIZIAJI VIUADUDU KUDHIBITI MALARIA

    June 17, 2025
  • KIBAHA DC YAVUKA MALENGO YA MAPATO, YAKAMILISHA MIRADI YOTE YA MAENDELEO

    June 16, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Kuzindua bunge
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TOVUTI YA MKOA WA PWANI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA AJIRA
  • TOVUTI YA WANANCHI
  • TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI
  • TOVUTI YA WIZARA YA AFYA
  • TOVUTI YA EWURA

Tovuti Zinazoshabihiana

  • TAMISEMI
  • MKOA WA PWANI
  • TANZANIA
  • AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    KIBAHA DISTRICT COUNCIL

    Anwani ya Posta: P.O BOX 30153

    Simu ya Mezani: +255 23240224

    Simu: +255 0767520048

    Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM)
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.