• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kibaha District Council
Kibaha District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

  • Mwanzo
    • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • SP FINAL DRAFT
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasmali Watu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Usimamizi wa Sheria
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sehemu ya Mifugo
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uchumi na Mipango
      • Maadili
      • UKIMWI
      • Huduma za Jamii
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Wafugaji Acheni Kutumia Silaha, Bunduki Kinyume na Sheria -DC Kibaha

Posted on: June 15th, 2022

KamatiI ya Usalama wilaya ya Kibaha ,imetoa onyo na kupiga marufuku baadhi ya wafugaji wanaodaiwa kutumia vibaya silaha ya bunduki na kutishia wasio na hatia ,kwani kwa kufanya hivyo ni uvunjifu wa amani na kinyume Cha matumizi.
Aidha imerejea onyo Hilo, kwa matumizi mabaya ya silaha za jadi Kama mishale na upinde na endapo kutatokea tukio la aina hiyo kamati hiyo haitosita kukomesha matumizi ya silaha hizo.
Mkuu wa wilaya ya Kibaha ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Usalama wilaya,Sara Msafiri alitoa maagizo hayo baada ya kufika Kijiji Cha Kitomondo ,Kata ya Ruvu Mkoani Pwani na kupata taarifa juu ya baadhi ya wafugaji wavamizi wanaotishia wakulima na wafugaji wengine kwa silaha mbalimbali huku wakiingiza mifugo kiholela kutoka ng'ambo.
Alisema ,kibali Cha kumiliki silaha hakiruhusu Raia kutishia Raia mwingine silaha ,hivyo waaanza kutafakari umiliki wa silaha kwa watu wa aina hiyo .
"Migogoro yenu malizeni kwa kukaa chini na kuheshimiana,bila ya kutumia bunduki,mishale Wala upinde."
Sara alisema ,anayachukua majina ya waliohusika na tukio Hilo ili vyombo vya sheria vikaendelee na uchunguzi na kuchukuliwa hatua ili iwe fundisho ndani ya jamii.
"Acheni kuweka sheria mfukoni,achane kudharau vyombo vya sheria, kisa rushwa ,"sitovumilia mambo haya katika wilaya hii,";Natoa Rai na kwa Serikali za vijiji, maofisa mifugo kufuata na kusimamia Utaratibu wa wafugaji kuingia katika vijiji ."alisisitiza.
"Kuna wasiwasi hapa ,Kuna mianya ya rushwa ndio inayotafuna Kijiji haiwezekani wafugaji wanaingia watakavyo na kuweka sheria mifukoni wakati wananchi mpo na Serikali ya Kijiji na kata mpo"
Pamoja na hayo,Sara alikemea mifugo holela na kuagiza Serikali ya kijiji cha Kitomondo kukutana na wafugaji wiki ijayo ili kubaini wafugaji wavamizi na idadi ya wafugaji wanaotambuliwa kuomba kibali Halali kwa mkutano wa Kijiji .
Vilevile mkuu huyo wa wilaya ,aliielekeza kamati ya usuluhishi ya kijiji na ofisa mifugo kupitia maboma yote ili kubaini wananchi wanaokodisha wafugaji ardhi .
Aliwataka wananchi kuheshimu juhudi za Serikali wakati ikileta Suluhu na kusimamia changamoto za wakulima na wafugaji wao wanakwenda kuwakumbatia wafugaji na kuwakodisha ardhi Hali inayosababisha migogoro isiyoisha.
Wakulima wa Kitomondo ,Kidawa Omary ,Hamza Botea Walisema ,kumezuka wimbi la mifugo na wafugaji wavamizi Hali inayosababisha kuliwa mazao Yao na kupata hasara .
Kidawa alisema , mfugaji Dotto Mabula ana maboma mengi ya Mifugo na ndio tishio la wafugaji.
Mfugaji Michael Mjika alisema ,Chama Cha wafugaji huwa kina kutana na kujadili changamoto zao ,ambapo amekiri kuwepo kwa wafugaji wavamizi na ambao wanakiuka taratibu na sheria mbalimbali.
Michael Lobe ambae amepigwa na baadhi ya watu waliotumwa na mfugaji ambae amedaiwa kuwa mbabe Dotto Mabula alisema, Juni 9 alivamiwa na kupigwa na kutishiwa bunduki wakati alipokwenda kumtembelea mkulima mmoja ambae amemkodisha ardhi kuweka mifugo.
Ofisa mifugo kata ya Ruvu ,Fransis Ekoni alipokea maagizo hayo na kusema wafugaji wanaotambulika katika kijiji cha Kitomondo ni wanne tu.
Ombeni Msangi kaimu mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kibaha,alieleza kuwa, kuingiza mifugo eneo jingine, Kijiji kingine kwa wakulima ni kosa.

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI WA BVR HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA January 23, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • MABADILIKO YA TAREHE YA USAILI September 24, 2024
  • Angalia Vyote

Matukio mapya

  • KAIMU KATIBU TAWALA WILAYA YA KIBAHA ATOA WITO KWA WENYEVITI WA MJI MDOGO MLANDIZI KUZINGATIA UADILIFU

    February 11, 2025
  • MAKAMU WA RAIS AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, ATOA WITO DHIDI YA UBADHILIFU

    April 02, 2025
  • ELIMU YA LISHE JUU YA USINDIKAJI WA BIDHAA ZA VYAKULA YATOLEWA KIBAHA DC.

    March 23, 2025
  • Mwenyekiti wa Halmashauri Amshukuru Rais Samia kwa Fedha za Miradi

    February 05, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Kuzindua bunge
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TOVUTI YA MKOA WA PWANI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA AJIRA
  • TOVUTI YA WANANCHI
  • TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI
  • TOVUTI YA WIZARA YA AFYA
  • TOVUTI YA EWURA

Tovuti Zinazoshabihiana

  • TAMISEMI
  • MKOA WA PWANI
  • TANZANIA
  • AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    KIBAHA DISTRICT COUNCIL

    Anwani ya Posta: P.O BOX 30153

    Simu ya Mezani: +255 23240224

    Simu: +255 0767520048

    Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM)
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.