Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha Butamo Ndalahwa amekabidhi vyeti vya pongezi pamoja na zawadi kwa waalimu wakuu wa shule za msingi waliongia kumi bora kiwilaya katika matokeo ya darasa la saba 2022.Akiongea wakati wa kukabidhi vyeti Butamo amewapongeza sana waalimu hao kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuwalea watoto kielimu na kimaadili."Niwapongeze kwa kazi kubwa mnayoifanya kwani matokea tunayoyaona ni juhudi zenu waalimu ." Alisema NdalahwaPamoja na pongezi hizo Butamo aliwataka waalimu hao kuhakikisha wanawalea watoto kimaadili pia kwani watoto hawewezi kufanya vizuri kimasomo kama hawana maadili.Aidha Butamo aliipongeza idara ya Elimu msingi kwa ufuatiliaji wanaofanya mara kwa mara mashuleni ."Niipongeze idara ya elimu msingi kwa ufuatiliaji wa mara kwa mara kwani kwa kufanya hivyo kunawafanya waalimu wanakuwa wawajibikaji n hii itafanya elimu ya Kibaha kupaa."Afisa Elimu kata ya Mlandizi Blandina Mwenura ambae shule tatu zilizoingia kumi bora zinatoka kwenye kata yake amesema ufuatiliaji wa mara kwa mara ndio ulifanikisha shule zake kufanya vizuri kiwilaya hadi kitaifa.Blandina amesema amekuwa akiwachukua waalimu na kupanga nao mbinu mbali mbali za kufundisha .Nae mwalimu Jovita kakulu wa shule ya msingi Muunga no ambae shule yake haijaingia kumi bora amesema ameshaunda klabu za kimasomo ambazo waalimu wanajumuika pamoja kuwasaidia wanafunzi.Awali akimkaribisha Mkurugenzi kwenye hafla fupi ya kukabidhi vyeti na zawadi iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri Afisa Elimu msingi Deogratious Mapunda amesema lengo la hafla hiyo ni kuwapongeza waalimu waliofanya vizuri na kutoa motisha kwa shule nyingine kufanya vizuri zaidi
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.