• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kibaha District Council
Kibaha District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

  • Mwanzo
    • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • SP FINAL DRAFT
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasmali Watu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Usimamizi wa Sheria
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sehemu ya Mifugo
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uchumi na Mipango
      • Maadili
      • UKIMWI
      • Huduma za Jamii
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

RC Aingilia Kati Mgogoro Dutumi

Posted on: September 27th, 2018

MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ameingilia kati mgogoro kati ya uongozi wa Kijiji cha Dutumi wilaya ya Kibaha na baadhi ya wajumbe wa Serikali ya Kijiji na wananchi


Mgogoro huo ambao umedumu kwa zaidi ya miezi saba walalamikaji walifikia hatua ya kumuamdikia rais barua kumielezea tuhuma za mwenyekiti wao Mkali Kanusu.


Kutokana na hali hiyo imemlazimu mkuu wa mkoa kuingilia kati na kuunda kamati ya watu watano ambao watafanya uchunguzi wa tuhuma za mwenyekiti na ikibainika hatua ziweze kuchukuliwa.


Akiongea na wananchi wa Kijiji cha Dutumi jana Mhandisi Ndikilo alisema, shughuli za maendeleo katika Kijiji hicho zimesimama kwa muda mrefu hivyo kamati hiyo italazimika kufanya kazi haraka ili ufumbuzi utafutwe kwa watakaobainika kuwa na tuhuma.


Kamati iliyoundwa ni pamoja na Kamanda wa polisi, Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mwanasheria, Ofisi ya Usalama wa Taifa (RCO) na mwakilishi kutoka ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Kibaha.


Alisema kamati hiyo itafanya kazi ndani ya siku saba ikibaini kuwa mwenyekiti ana tuhuma za kujibu, Mtendaji wa Kijiji atamuandikia mkuu wa Wilaya barua ambae nae ataandika barua kwa mwenyekiti wa Kijiji ambae atapewa muda wa kujibu baada ya majibu hayo Mkuu wa mkoa atatoa maelekezo kwa Serikali ya Kijiji.


Katika barua iliyoandikwa na baadhi ya wananchi hao kwenda kwa Rais John Magufuli ilieleza kuwa mwenyekiti anatuhumiwa kuhusika na ubadhilifu wa fedha, kupokea wawekezaji tofauti na waliopitishwa, lakini pia barua hiyo ilimtuhumu mbunge wa Kibaha Vijijini kuhusika na tukio la kupiga risasi tano hewani kuwatisha wananchi.


Barua hiyo ilieleza kuwa siku moja kabla ya mahojiano na maofisa wa TAKUKURU ndipo usiku ilisikika risasi zikipigwa hewani ambazo walihofia ni za kuwatisha wananchi wasijitokeze kutoa ushirikiano dhidi ya tuhuma za mwenyekiti wao kwenye ubadhilifu wa fedha za Kijiji.


Hata hivyo Mhandisi Ndikilo alisema, tuhuma hizo zimeanza kufanyiwa kazi na Jeshi la Polisi ikibainika hatua za kisheria zitachukiliwa.


Aidha alisema, ikibainika tuhuma ni za uongo wahusika watachukuliwa hatua, aliwaomba pia wananchi kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa kamati hiyo ili kurahisisha zoezi.


Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mkali Kanusu alisema, hahusiki na tuhuma hizo na badala yake ni njama za kikundi cha watu wachache ambao wanalenga kumchafua, hata hivyo ameahidi kutoa ushirikiano kwa kamati iliyoundwa pale itakapomhitaji.


Mmoja wa wannchi hao Said Muhode alisema baadhi ya wajumbe wa Kijiji wamekua chanzo cha mgogoro katika Kijiji hicho.


Abdalla Mwinyimvua alisema, wawekezaji waliopo sio waliopitishwa hali inayoendeleza migogoro katika Kijiji hicho.


Kijiji hicho mgogoro wake ulianza kutatuliwa na mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpta Mshama na baadae mkuu wa mkoa kuingilia kati baada ya kuona baadhi ya shughuli zinakwama kutikana na kutokua na maelewano kati ya mwenyekiti na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Kijiji.


Matangazo

  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI WA BVR HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA January 23, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • MABADILIKO YA TAREHE YA USAILI September 24, 2024
  • Angalia Vyote

Matukio mapya

  • WWF YAKABIDHI MICHE YA MICHIKICHI KUHIFADHI KINGO ZA MTO RUVU

    May 24, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU NA UWEKAJI WAZI TAARIFA ZA MPIGA KURA AWAMU YA PILI YAFANYIKA KIBAHA

    May 14, 2025
  • WATAALAM WA AFYA PWANI WAKUTANA KUJADILI KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA WATOTO WACHANGA

    May 14, 2025
  • VIONGOZI WA VYAMA SIASA WARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA MKUU WA WILAYA NA MKURUGENZI MTENDAJI KIBAHA DC

    May 07, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Kuzindua bunge
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TOVUTI YA MKOA WA PWANI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA AJIRA
  • TOVUTI YA WANANCHI
  • TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI
  • TOVUTI YA WIZARA YA AFYA
  • TOVUTI YA EWURA

Tovuti Zinazoshabihiana

  • TAMISEMI
  • MKOA WA PWANI
  • TANZANIA
  • AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    KIBAHA DISTRICT COUNCIL

    Anwani ya Posta: P.O BOX 30153

    Simu ya Mezani: +255 23240224

    Simu: +255 0767520048

    Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM)
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.