• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kibaha District Council
Kibaha District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

  • Mwanzo
    • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • SP FINAL DRAFT
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasmali Watu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Usimamizi wa Sheria
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sehemu ya Mifugo
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uchumi na Mipango
      • Maadili
      • UKIMWI
      • Huduma za Jamii
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU NA UWEKAJI WAZI TAARIFA ZA MPIGA KURA AWAMU YA PILI YAFANYIKA KIBAHA

Posted on: May 14th, 2025

Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha imeendesha mafunzo ya awamu ya pili kuhusu uandikishaji na uwekaji wazi wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Mei 16, 2025 katika Ukumbi wa NMB Mlandizi, yakiwa yamefunguliwa rasmi na Afisa Mwandikishaji ngazi ya Jimbo,

Bi. Regina L. Bieda.


Akizungumza wakati wa ufunguzi, Bi. Bieda amewataka washiriki kuzingatia mafunzo hayo kwa umakini ili kwenda kutekeleza majukumu yao kwa weledi, huku wakifuata Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania.

Kwa nyakati tofauti, Maafisa TEHAMA kutoka Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania, Bw. Richard Simon na Bw. Paul Mpangala, wamehimiza washiriki kuhakikisha wanatumia mafunzo hayo kama msingi wa utekelezaji wa kazi kwa kuzingatia misingi ya haki, sheria na kanuni za uchaguzi.

Kwa upande wake, Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Bi. Grace Haule, amesema kuwa kutakuwa na jumla ya vituo 19 vya kuhakiki taarifa za wapiga kura katika Halmashauri hiyo, ambapo kila kata itakuwa na angalau kituo kimoja. Aidha, kwa kata zenye idadi kubwa ya watu, vituo vitakuwa viwili hadi vitatu ili kurahisisha zoezi hilo kufanyika kwa ufanisi.


Bi. Haule amewahamasisha wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kujitokeza kwa wingi katika vituo walivyojiandikishia awali, ili kuhakiki taarifa zao kwenye daftari hilo.


Mafunzo hayo yamehitimishwa kwa hotuba ya Afisa Mwandikishaji ambaye amesisitiza kuwa washiriki watumie mafunzo hayo kama nyenzo muhimu katika utekelezaji wa majukumu yao, na pia wahamasishe wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la uboreshaji wa daftari litakalofanyika kuanzia Mei 16 hadi Mei 22, 2025.

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI WA BVR HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA January 23, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • MABADILIKO YA TAREHE YA USAILI September 24, 2024
  • Angalia Vyote

Matukio mapya

  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU NA UWEKAJI WAZI TAARIFA ZA MPIGA KURA AWAMU YA PILI YAFANYIKA KIBAHA

    May 14, 2025
  • WATAALAM WA AFYA PWANI WAKUTANA KUJADILI KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA WATOTO WACHANGA

    May 14, 2025
  • VIONGOZI WA VYAMA SIASA WARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA MKUU WA WILAYA NA MKURUGENZI MTENDAJI KIBAHA DC

    May 07, 2025
  • ELIMU YA USALAMA BARABARANI YATOLEWA KWA MADEREVA NA WATUMISHI WA UMMA KIBAHA DC

    May 13, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Kuzindua bunge
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TOVUTI YA MKOA WA PWANI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA AJIRA
  • TOVUTI YA WANANCHI
  • TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI
  • TOVUTI YA WIZARA YA AFYA
  • TOVUTI YA EWURA

Tovuti Zinazoshabihiana

  • TAMISEMI
  • MKOA WA PWANI
  • TANZANIA
  • AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    KIBAHA DISTRICT COUNCIL

    Anwani ya Posta: P.O BOX 30153

    Simu ya Mezani: +255 23240224

    Simu: +255 0767520048

    Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM)
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.