• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kibaha District Council
Kibaha District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

  • Mwanzo
    • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • SP FINAL DRAFT
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasmali Watu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Usimamizi wa Sheria
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sehemu ya Mifugo
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uchumi na Mipango
      • Maadili
      • UKIMWI
      • Huduma za Jamii
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Madeni ya Watumishi na Wazabuni Kupewa Kipaumbele

Posted on: August 30th, 2023

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kibaha hadi kufika Juni 30, 2023, ilikuwa imekusanya na kupokea mapato pamoja bakaa Jumla ya Sh. Biln 31,960,714,473.62 Sawa na asilimia 85.78 ya maksio ya Sh. Biln 37,257,763,726.72 .


Hayo yamebainishwa na Mweka hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Zubeda Nkala alipokuwa akiwasilisha hesabu za mwisho ( final accounts) za Halmashauri zinazoishia Juni 30, 2023 katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani la kujadili taarifa hizo.


Zubeda amesema pamoja na kukusanya kiasi cha Bilion 31.960 Halmashauri imetumia sh. Bilion 25,895,087,172 Sawa na asilimia 81 ya mapato yaliyopokelewa.


Kwa mujibu wa Zubeda  mapato yameongezeka kwa asilimia 9.65 kutoka Sh. Biln.29,146,982,035 mwaka 2021/2022 hadi Sh.Biln. 31,960,714,473 kwa mwaka 2022/2023


Aidha Mweka hazina huyo ameeleza katika kikao hicho kwamba  Halmashauri intarajia kujenga soko la kisasa katika eneo la Mlandizi ili kuwezesha wananchi kupata huduma bora karibu na wanakoishi.


Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Pwani Mwajuma Mohamed ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kuongeza mapato tofauti na miaka ya nyuma na kuwataka waendelee kuboresha mikakati ya ukusanyaji.


"Nawapongeza kwa kupandisha makusanyo tofauti na miaka ya nyuma najua juhudi mbali mbali zimefanyika wiki iliyopita tulikuwa hapa na GIZ tukifundishwa tukiandaa mikakati mbali mbali ya kuongeza mapato katika Halmashauri hii niwaombe mkazingatie yote tuliyokubaliana " amesema Mwajuma.


Mwajuma amesema lazima hatua stahiki zichukuliwe kwa wadaiwa wa viwanja kulingana na mkataba kwani watu wamekuwa wakishilia viwanja vya Halmashauri kwa zaidi ya miaka sita bila kulipa hivyo alimtaka mwanasheria kusimamia mkataba wa mauzo ya viwanja hivyo.


Akifunga kikao hicho Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mhe. Mwinshehe Shomari amempongeza Mwekahazina kwa maandalizi mazuri ya kitabu hicho kwani kimeandaliwa kwa ufupi kila anaesoma anaelewa .


Vilevile Shomari amesema swala la ukusanyaji wa mapato ni kipaumbele chao na wanatimu imara ya mapato ambayo inafanya kazi kwa ufanisi hadi kupelekea kupanda kwa mapato kwa mwaka 2022/2023.


Amesema swala la kulipa madeni kwa watumishi na wazabuni wamelipa kipaumbele na walishaagiza kila robo taarifa za madeni zitakuwa zinawasilishwa.

Pamoja na kulipa madeni pia wanafuatilia vikundi vyote vilivyochukua mkopo wa Halmashauri na bado hawajarejesha.


Makamu Mwenyekiti  huyo amesema wameshaanza kuchukua hatua za kuvipeleka vikundi hivyo mahakamani.

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI WA BVR HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA January 23, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • MABADILIKO YA TAREHE YA USAILI September 24, 2024
  • Angalia Vyote

Matukio mapya

  • KAIMU KATIBU TAWALA WILAYA YA KIBAHA ATOA WITO KWA WENYEVITI WA MJI MDOGO MLANDIZI KUZINGATIA UADILIFU

    February 11, 2025
  • MAKAMU WA RAIS AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, ATOA WITO DHIDI YA UBADHILIFU

    April 02, 2025
  • ELIMU YA LISHE JUU YA USINDIKAJI WA BIDHAA ZA VYAKULA YATOLEWA KIBAHA DC.

    March 23, 2025
  • Mwenyekiti wa Halmashauri Amshukuru Rais Samia kwa Fedha za Miradi

    February 05, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Kuzindua bunge
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TOVUTI YA MKOA WA PWANI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA AJIRA
  • TOVUTI YA WANANCHI
  • TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI
  • TOVUTI YA WIZARA YA AFYA
  • TOVUTI YA EWURA

Tovuti Zinazoshabihiana

  • TAMISEMI
  • MKOA WA PWANI
  • TANZANIA
  • AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    KIBAHA DISTRICT COUNCIL

    Anwani ya Posta: P.O BOX 30153

    Simu ya Mezani: +255 23240224

    Simu: +255 0767520048

    Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM)
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.