• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kibaha District Council
Kibaha District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

  • Mwanzo
    • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • SP FINAL DRAFT
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasmali Watu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Usimamizi wa Sheria
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sehemu ya Mifugo
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uchumi na Mipango
      • Maadili
      • UKIMWI
      • Huduma za Jamii
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

KIBAHA DC YAPAZA SAUTI DHIDI YA UKATILI KWA WATOTO KATIKA MAADHIMISHO YA MTOTO WA AFRIKA

Posted on: June 16th, 2025

Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha imeungana na mataifa mengine barani Afrika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika kwa kuhimiza ulinzi wa haki za watoto na malezi bora katika jamii.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo, tarehe 16 Juni 2025, katika ukumbi wa NMB uliopo Mlandizi, yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wazazi, walimu pamoja na watoto kutoka maeneo tofauti ya Halmashauri hiyo.


Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Bi. Halima Jongo ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, ametoa wito kwa wazazi na jamii kwa ujumla kuhakikisha watoto wanalelewa katika maadili mema na mazingira salama ili waweze kuwa nguzo imara ya maendeleo ya Taifa.

“Natoa rai kwa jamii yote kuwajibika katika kuhakikisha watoto wanapata malezi bora, elimu sahihi na kinga dhidi ya vitendo vyote vya ukatili. Hili ni jukumu letu sote kama wazazi, walezi na viongozi,” alisema Bi. Jongo.


Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Bi. Grace Haule, alieleza kuwa kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii, Halmashauri inapanga kuanzisha Mabaraza ya Watoto yatakayosaidia kutoa fursa kwa watoto kueleza changamoto zao na kushirikiana katika kuzitafutia suluhisho.


Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri hiyo, Bw. Yahaya Mbogolume, amesisitiza umuhimu wa malezi yanayozingatia Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009, akibainisha kuwa uelewa wa sheria hiyo utasaidia kupunguza ukatili dhidi ya watoto.


Aidha, Afisa Lishe wa Halmashauri, Bi. Coletha Chapile, aliwahimiza wazazi kuhakikisha watoto wanapata lishe bora kwa lengo la kupunguza viwango vya udumavu vinavyolikabili Taifa.

Nao Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia chini ya Inspekta Tumaini Steven Ulimboka, limewahimiza watoto na wazazi kuripoti mara moja vitendo vyote vya ukatili ili viweze kufanyiwa kazi kisheria.

Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa kila mwaka tarehe 16 Juni kwa kumbukumbu ya mauaji ya watoto wa Kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini mwaka 1976, waliouawa wakidai haki ya elimu bora. Umoja wa Afrika ulipitisha maadhimisho haya mwaka 1990 kwa lengo la kuendeleza juhudi za kupinga ukatili na kukuza ustawi wa watoto barani Afrika.

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI WA BVR HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA January 23, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • MABADILIKO YA TAREHE YA USAILI September 24, 2024
  • Angalia Vyote

Matukio mapya

  • JUKWAA LA WANAWAKE KIBAHA DC LAFANYA UCHAGUZI, DKT. MAIMUNA AIBUKA MWENYEKIT

    June 23, 2025
  • MADIWANI KIBAHA WAAGWA RASMI, MAFANIKIO YASISITIZWA KAMA URITHI WA USHIRIKIANO

    June 20, 2025
  • HALMASHAURI YA KIBAHA YAZINDUA ZOEZI LA UNYUNYIZIAJI VIUADUDU KUDHIBITI MALARIA

    June 17, 2025
  • KIBAHA DC YAVUKA MALENGO YA MAPATO, YAKAMILISHA MIRADI YOTE YA MAENDELEO

    June 16, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Kuzindua bunge
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TOVUTI YA MKOA WA PWANI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA AJIRA
  • TOVUTI YA WANANCHI
  • TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI
  • TOVUTI YA WIZARA YA AFYA
  • TOVUTI YA EWURA

Tovuti Zinazoshabihiana

  • TAMISEMI
  • MKOA WA PWANI
  • TANZANIA
  • AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    KIBAHA DISTRICT COUNCIL

    Anwani ya Posta: P.O BOX 30153

    Simu ya Mezani: +255 23240224

    Simu: +255 0767520048

    Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM)
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.