• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kibaha District Council
Kibaha District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

  • Mwanzo
    • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • SP FINAL DRAFT
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasmali Watu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Usimamizi wa Sheria
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sehemu ya Mifugo
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uchumi na Mipango
      • Maadili
      • UKIMWI
      • Huduma za Jamii
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

KIBAHA DC YAIMARISHA UFANISI KWA WATUMISHI KUPITIA MAFUNZO YA MFUMO WA ESS

Posted on: June 12th, 2025

Katika kuhakikisha ufanisi na uwajibikaji kwa watumishi wa umma, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha imeendesha mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa Utumishi wa Umma (ESS) kwa watumishi wake wote, yaliyofanyika tarehe 11 Juni 2025 katika Ukumbi  wa Halmashauri hiyo.

Akifungua rasmi mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Bi. Regina L. Bieda, amewataka watumishi kutumia mfumo huo kwa weledi na kujaza majukumu yao ya kila siku kwa usahihi, ili kuimarisha utendaji kazi na kuwezesha tathmini sahihi ya uwajibikaji wao.
“Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira rafiki ya kazi kupitia mfumo huu wa ESS, lengo likiwa ni kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa mtumishi na kuongeza ufanisi katika sekta ya umma,” alisema Bi. Bieda.

Kwa upande wake, Afisa TEHAMA wa Halmashauri hiyo, Bw. Menard Mvimbile, amesisitiza umuhimu wa kufuata maelekezo ya matumizi ya mfumo huo na kuwahimiza watumishi wote kuwasiliana na idara husika pindi wanapokutana na changamoto zozote.
Bw. Mvimbile alitoa mafunzo ya namna ya kujaza majukumu ya kila siku pamoja na taratibu za kuwasilisha maombi ya likizo kwa njia ya kielektroniki kupitia mfumo wa ESS.

Aidha, Afisa  Utumishi wa Halmashauri Edward Masona  aliwataka watumishi kuzingatia maadili ya kazi, kutokujihusisha na vitendo vya rushwa, uzembe na uchelewaji kazini, akibainisha kuwa mfumo huu utaongeza uwazi na uwajibikaji.

Watumishi waliopata fursa ya kushiriki mafunzo hayo, akiwemo Janeth Mndeme na Abel Mlelwa, wameeleza kufurahishwa na mafunzo hayo wakisema yamewajengea uelewa mpana kuhusu matumizi ya mfumo wa ESS, tofauti na awali ambapo walikuwa na changamoto nyingi katika kuutumia.
Mafunzo hayo ya siku moja yalihitimishwa kwa Mkurugenzi Bi. Regina L. Bieda kukusanya changamoto zote zilizowasilishwa na kuahidi kuzifanyia kazi kwa kushirikiana na taasisi husika ili kuhakikisha mfumo unafanya kazi kwa tija na ufanisi mkubwa zaidi.

Matangazo

  • MAONESHO YA NANE NANE KANDA YA MASHARIKI YANATARAJIWA KUANZA RASMI TAREHW 01.08.2025 WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA July 18, 2025
  • Tarehe 31.07.2025 MHESHIMIWA RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN ATAZINDUA BANDARI KAVU YA KWALA WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA July 28, 2025
  • Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuzindua bandari kavu Kwala tarehe 31.07.2025 July 25, 2025
  • Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuzindua bandari kavu Kwala tarehe 31.07.2025 July 25, 2025
  • Angalia Vyote

Matukio mapya

  • KWALA YAANDIKA HISTORIA MPYA, RAIS SAMIA AZINDUA SAFARI ZA MIZIGO SGR NA BANDARI KAVU MKOANI PWANl

    July 31, 2025
  • KWALA YAANDIKA HISTORIA MPYA: BANDARI KAVU, VIWANDA NA TRENI YA MIZIGO KUZINDULIWA NA RAIS SAMIA KESHO

    July 30, 2025
  • MANAGEMENT YA HALASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA YATEMBELEA BANDARI KAVU KWALA

    July 28, 2025
  • MANAGEMENT YA HALASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA YATEMBELEA BANDARI KAVU KWALA

    July 28, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Kuzindua bunge
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TOVUTI YA MKOA WA PWANI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA AJIRA
  • TOVUTI YA WANANCHI
  • TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI
  • TOVUTI YA WIZARA YA AFYA
  • TOVUTI YA EWURA

Tovuti Zinazoshabihiana

  • TAMISEMI
  • MKOA WA PWANI
  • TANZANIA
  • AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    KIBAHA DISTRICT COUNCIL

    Anwani ya Posta: P.O BOX 30153

    Simu ya Mezani: +255 23240224

    Simu: +255 0767520048

    Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM)
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.