• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kibaha District Council
Kibaha District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

  • Mwanzo
    • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • SP FINAL DRAFT
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasmali Watu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Usimamizi wa Sheria
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sehemu ya Mifugo
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uchumi na Mipango
      • Maadili
      • UKIMWI
      • Huduma za Jamii
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha yakabidhiwa Gari la Wagonjwa

Posted on: January 26th, 2024

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kibaha imepokea gari ya wagonjwa ambayo itatumika katika Hospitali ya Wilaya hiyo na kuondoa kero iliyokuwepo awali iliyosababishwa na uhaba wa magari hayo.


Kwasasa Halmashauri ya Wilaya Ina magari manne ya wagonjwa awali changamoto zaidi ilikuwa katika kituo cha afya Mlandizi ambacho kipo Mjini na kinahudumia wagonjwa wengi zaidi


Akikabidhi gari hilo kwa  Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Michael Mwakamo  alitaka gari hilo kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa Ili lidumu kwa muda mrefu.


Mwakamo  aliwataka watendaji kutotumia gari hilo kama daladala kwa ajili ya kwenda kazini badala yake waendelee kutumia bajaji na usafiri mwingine.


"Gari hili linakuja kuondoa changamoto ya uhaba wa magari iliyokuwepo awali, litumike kwa malengo yaliyokusudiwa Ili kuendelea kuwasaidia wagonjwa," alisema.


Mwakamo alijivunia jitihada zake za kuleta maendeleo katika Jimbo hilo huku akiishukuru Serikali kwa namna inavyotoa fedha na vitendea kazi kumaliza kero za Wananchi.


Ametaka pia Wananchi kuwapima viongozi kwa kazi wanazofanya hususani za kuondoa vikwazo vya maendeleo kwenye maeneo yao kama inavyofanya Serikali ya awamu ya sita.


" Rais Dk.Samia Suluhu Hassan tunamshukuru kwa namna ambavyo ameendelea kubadilisha Jimbo letu kwa maendeleo kila sekta ameigusa anatufanya tujivunie kwa wananchi wetu " alieleza.


Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dk.Wilford Kondo alisema kwamba hakuna mgonjwa atakayetizwa fedha kwa huduma ya gari hilo la wagonjwa na kwamba atakayedaiwa fedha ya mafuta atoe taarifa.


 Dk Kondo aliwataka Wananchi kufika kupata huduma katika Hospitali ya Wilaya kwani huduma nyingi kwasasa zinapatikana katika Hospitali hiyo tofauti na awali ambapo ilikuwa lazima mgonjwa apewe rufaa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.


Diwani wa Mlandizi Euphrasia Kadala akiishukuru Serikali kwa kutoa gari hilo la wagonjwa kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya  ambalo sasa litakwenda kuondoa adha ya kukodi magari pindi lililopo linapopata hitilafu.


Tatu Haji na John Pilly ni wakazi wa Mlandizi ambao wanaishukuru Serikali kwa ajili ya gari hilo litakalosaidia kuhudumia wagonjwa kwa haraka.


Mwisho

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI WA BVR HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA January 23, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • MABADILIKO YA TAREHE YA USAILI September 24, 2024
  • Angalia Vyote

Matukio mapya

  • KAIMU KATIBU TAWALA WILAYA YA KIBAHA ATOA WITO KWA WENYEVITI WA MJI MDOGO MLANDIZI KUZINGATIA UADILIFU

    February 11, 2025
  • MAKAMU WA RAIS AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, ATOA WITO DHIDI YA UBADHILIFU

    April 02, 2025
  • ELIMU YA LISHE JUU YA USINDIKAJI WA BIDHAA ZA VYAKULA YATOLEWA KIBAHA DC.

    March 23, 2025
  • Mwenyekiti wa Halmashauri Amshukuru Rais Samia kwa Fedha za Miradi

    February 05, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Kuzindua bunge
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TOVUTI YA MKOA WA PWANI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA AJIRA
  • TOVUTI YA WANANCHI
  • TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI
  • TOVUTI YA WIZARA YA AFYA
  • TOVUTI YA EWURA

Tovuti Zinazoshabihiana

  • TAMISEMI
  • MKOA WA PWANI
  • TANZANIA
  • AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    KIBAHA DISTRICT COUNCIL

    Anwani ya Posta: P.O BOX 30153

    Simu ya Mezani: +255 23240224

    Simu: +255 0767520048

    Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM)
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.