• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kibaha District Council
Kibaha District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • SP FINAL DRAFT
      • Mazingira na Usafishaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maji
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Ufugaji wa Nyuki
      • Uchaguzi
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Maji
    • Afya
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uchumi na Mipango
      • Maadili
      • UKIMWI
      • Huduma za Jamii
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Halmashauri ya Wilaya ya kibaha Inaendesha Kampeni ya Siku ya Utoaji wa Chanjo ya Polio

Posted on: November 23rd, 2022

Halmashauri ya wilaya ya Kibaha inaendesha kampeni ya siku 7 ya utoaji wa chanjo ya Uviko-19  kwa watu wote wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea  iliyoanza tarehe 25/11/2022  hadi tarehe 30/11/2022, pamoja na chanjo ya ugonjwa wa Polio kwa watoto wenye umri kuanzia 0 hadi miaka 4 kampeni ya chanjo ya polio itaanza tarehe 1/12/2022 hadi tarehe 4/12/2022.

Katibu Tawala Wilaya ya Kibaha Sozy Ngate amesema  Dhamira ya Serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na afya njema hivyo  Wilaya ya Kibaha  kwa pamoja imejipanga kuhakikisha inafikisha asilimia 100 ya chanjo ya UVIKO kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya Kibaha kwa kuendelea kutoa elimu na kufanya uhamasishaji wa kutosha.

Katibu Tawala ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa kamati ya msingi ya Afya ngazi ya jamii (PHC)yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri yakiwa na  lengo la kuwajengea uwezo kuhusu chanjo ya Uviko 19 na chanjo ya polio.

Aidha  Sozy amewataka wazazi kuwapeleka watoto wao kupata chanjo ya polio kwani chanjo hii inatolewa ili kuwapa uimara watoto wao katika kujikinga na ugonjwa wa polio ambao hauna tiba na baadhi ya madhara ya ugonjwa huu ni pamoja na kuleta athari katika mfumo wa fahamu wa mtoto na kupooza. Serikali inafanya jitihada mbalimbali kuhakikisha watoto wote wanakuwa salama kiafya ndo maana kuna chanjo ya polio ambapo mtoto anapewa matone ya chanjo.

 

“ Katika kuhakikisha tunakamilisha lengo la kutoa chanjo kwa walengwa 18,525 ndani ya muda wa siku nne za Kampeni yaani tarehe 01/12 - 04/12/2022. Tumekubaliana kwa pamoja kutoa elimu kuhusu umuhimu wa chanjo ya polio na madhara yanayoweza kujitokeza kwa mtoto asiyepatiwa chanjo hiyo. Hivyo tuna imani tukishirikiana kwa pamoja tutafanikisha kwani toka awamu zilizopita za chanjo Halmashauri ya Wilaya Kibaha tulifanya vizuri”. Amesema Ngate

 

Mratibu wa chanjo halamshauri ya wilaya kibaha Khadija Telacky amewataka wananchi kuchanja chanjo ya uviko 19 kwani haina madhara na itwakinga na ugonjwa wa uviko 19  pia amewataka wazazi kuwapa ushirikiano wa kutosha wahudumu wa afya watakaopita kwenye nyumba zao na mitaa kwa kuwatoa watoto wote wenye umri kuanzia miaka0-4 ili waweze kupata chanjo ya polio kwani ugonjwa wa polio ni ugonjwa hatari .

Telacky amesema mpaka sasa kwa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha wameshachanja chanjo ya Uviko kwa asilimia 77 wanategemea kumaliza asilimia 33 zilizobaki ifikapo desemba 2022.

Pia mratibu huyo wa chanjo ameitaka kamati ya msingi ya afya kwenda kuwa mabalozi wazuri kwa jamii kuhusu chanjo ya uviko na polio

Mchungaji Chamade Horohoro ameahidi atakuwa balozi mzuri wa kuelimisha waumini umuhimu wa chanjo kwani binadamu anahitaji mambo matatu kwa ajili ya ustawi wake ambayo ni afya ya akili, utimamu wa mwili na uelewa sahihi hivyo akikosa kimojawapo atakuwa na mapungufu ndio maana nahamasisha jamii kuchanja ili wawe na utimamu wa mwili

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI May 25, 2023
  • TANGAZO LA KAZI YA MTUNZA KUMBUKUMBU June 01, 2023
  • Tangazo la Uuzaji wa Viwanja Lupunga June 22, 2021
  • TANGAZO KWA WATUMISHI AJIRA MPYA July 04, 2022
  • Angalia Vyote

Matukio mapya

  • MIRADI 99 YA MAENDELEO MKOA WA PWANI ILIYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU IMEPITA BILA DOSARI

    May 24, 2023
  • ANGOLA WATEMBELEA KIBAHA KUJIFUNZA KUHUSU TASAF

    May 28, 2023
  • Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Amezindua Zoezi la Chanjo

    April 25, 2023
  • JAFO AMEZINDUA KAMPENI YA MATUMIZI YA NISHATI MBADALA PWANI.

    April 17, 2023
  • Angalia Vyote

Video

Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Kuzindua bunge
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TOVUTI YA MKOA WA PWANI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA AJIRA
  • TOVUTI YA WANANCHI
  • TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI
  • TOVUTI YA WIZARA YA AFYA
  • TOVUTI YA EWURA

Tovuti Zinazoshabihiana

  • TAMISEMI
  • MKOA WA PWANI
  • TANZANIA
  • AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    KIBAHA DISTRICT COUNCIL

    Anwani ya Posta: P.O BOX 30153

    Simu ya Mezani: +255 23240224

    Simu: +255 0767520048

    Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM)
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.