Kiswahili
  • English
  • Kiswahili
    • Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kibaha District Council
Kibaha District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

  • Mwanzo
    • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • SP FINAL DRAFT
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasmali Watu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Usimamizi wa Sheria
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sehemu ya Mifugo
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uchumi na Mipango
      • Maadili
      • UKIMWI
      • Huduma za Jamii
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Imetekeleza Agizo la kisheria la Kutoa Asilimia kumi ya Mapato ya Ndani kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na watu Wenyenye Ulemavu

Posted on: February 11th, 2021

HALMASHAURI  WILAYA YA KIBAHA IMETEKELEZA AGIZO LA KISHERIA LA KUTOA ASILIMIA KUMI YA MAPATO YAKE YA NDANI KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU

 

Mamlaka za serikali za mitaa Tanzania zina wajibu ya kutenga 10% ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya Wanawake,Vijana  na Watu wenye Ulemavu.

Katika kuhakikisha hilo linafanikiwa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha imekuwa ikitenga asilimia 10% ya mapato yake ya ndani na kutoa mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Ambapo asilimia 4% huelekezwa kwa wanawake, asilimia 4%kwa vijana na asilimia 2% huelekezwa kwa watu wenye ulemavu.

 Ili kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa, wataalamu kutoka Idara ya Maendeleo ya Jamii  Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, wamekuwa  wakiwajengea uwezo kwanza kwa kuwapa elimu na mafunzo mbalimbali juu ya matumizi sahihi ya fedha hizo.

Mikopo hiyo imekuwa ikitolewa   kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia kamati ndogo za mikopo zilizoundwa katika ngazi ya kata na kuratibiwa na maafisa maendeleo ya Jamii kata na kupitishwa na kamati za Maendeleo za kata (WDC) na kisha kupitishwa katika vikao vya kamati za kudumu za Halmashauri. Awali fedha hizo za mkopo kwa makundi hayo mawili zilikuwa zikitolewa kwa masharti ya riba ya asilimia 10 kwa mwaka.

 Mwaka 2017 serikali iliziagiza mamlaka za serikali za mitaa kuongeza kundi la walemavu katika upatikanaji wa mikopo hiyo. Ili kuweza kuwasaidia Wanawake, vijana na walemavu kujikwamua kiuchum.

 Mwaka 2018 serikali ilitoa muongozo kuwa mikopo hiyo itolewe bila riba ili kuwapa fursa wanawake, vijana na watu wenye  ulemavu kwa ajili ya kuanzisha miradi kwa wingi ya kujikwamua kiuchumi kwani suala la riba limekuwa kikwazo kwa makundi mengi kuweza kukopa na kurejesha mikopo kwa wakati

Kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha ilitoa mikopo kwa vikundi 13 vya  Wanawake kiasi cha Tshs 46,315,000.

Mojawapo ya vikundi vya wanawake vilivyowezeshwa ni  Jawaba ambacho kina wanachama watano na kilipata mkopo wa Tshs 5,000,000. Kwa kupitia mkopo huo wameweza kuanzisha biashara ya kuuza mchele,kufuga kuku wa kisasa ambapo wana  jumla ya kuku 100 pamoja na kutengeneza sabauni za maji.

Wanakikundi hawa wanasema kupitia miradi waliyoanzisha wameweza kuwalipia watoto wao ada za shule na kuwapatia huduma za msingi.

Pamoja na hicho Kikundi kingine cha  wanawake kilichofaidika na mkopo ni kikundi cha  Mshikamano kinachojishughulisha na ubanguaji wa korosho na uuzaji wa korosho . kikundi hiki kina wanachama watano walipata mkopo wa Tsh 4,000,000.

Wanachama wa kikundi hiki wanashukuru serikali kwa kuwapatia mkopo usiokuwa na riba kwani kupitia mkopo huu wameweza kujikomboa kimaisha ikiwemo kusomesha watoto,kuboresha makazi yao ya kuishi kwani zamani walikuwa wanaishi kwenye mazingira duni lakini kupitia biashara wanayofanya wameboresha makazi hayo.

Vile vile Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha imeendelea kutoa mikopo kwa vijana, Kwa mwaka wa fedha 2019/2020 jumla ya Tshs 27,000,00 kilitolewa kwa vikundi 6 vya  vijana.

Mojawapo ya kikundi cha vijana kilichopata mkopo huo  ni kikundi cha tupendane vijana group kilichopo Kata ya Gwata ambacho kinawanachama 5 na kilipewa mkopo wa 5,000,000. Kikundi hiki kinajishughulisha na kutengeneza chanuo za mbao.

Mwenyekiti wa kikundi hicho anasema awali walikuwa wanatengeneza chanuo 500 lakini baada ya kupata mkopo kutoka halmashauri wameweza kutengeneza chanuo 2000 hadi 3000 kutegemea na soko.

Pamoja na kuongeza uzalishaji wameweza kuongeza biashara nyingine ikiwemo biashara ya pikipiki kwa sasa wanachama wa kikindi hiki wanamiliki pikipiki ambazo wamewapa vijana wengine wafanyie biashara na kuwaletea hesabu jioni.

 Aidha , Vijana hawa wanasema wameweza kuboresha makazi yao ya kuishi kwani walikuwa wameanza ujenzi lakini walikuwa hawajaweza kumalizia lakini baada ya kuanzisha bishara hii ya chanuo wameweza kumalizia ujenzi wa nyumba zao  hizo na vijana wengine waliokuwa wanaishi kwao wameweza kwenda kupanga na wanajitegemea .

Kikundi kingine cha vijana kichonufaika na mkopo kutoka Halmashauri  ni Pande group kilichopo Bokomnemela, kikundi hiki kilipata mkopo wa milioni nne na kina wanachama watano wanajishulisha na mradi wa stationary pamoja na saluni ya kiume.

Katibu wa kikundi hiki Ramadhani Bakari Msusa anasema kupitia mkopo huu wameweza kuboresha biashara yao kwa kuongeza vitendea kazi kama mashine ya kutolea kopi kwani mwanzo hawakuwa nayo, wameweza kuongeza mashine moja ya kunyolea pamoja na printa.

Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha imeendelea kuwawezesha watu wenye ulemavu kwa kuwapatia mkopo wenye masharti nafuu. Kwa mwaka wafedha 2018/ 2019 halmashauri iliwezesha vikundi 10 vya watu wenye ulemavu kiasi cha tsh 22,500,000  kutokana na kutokuwepo na vikundi vingi vya watu wenye ulimavu halmashauri haikuweza kutoa mkopo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Hata hivyo mwaka wa fedha 2020/2021 Halmashauri imeweza kutoa mkopo kwa vikundi ambavyo vimemaliza mkopo na kuomba tena jumla ya tsh 16,780,000 zilitolewa kwa vikundi saba.

Mojawapo ya kikundi kilichonufaika na mkopo wa watu wenye ulemavu ni Tunaweza group kilichopo mlandizi kina jumla ya wanachama watano na kilipata mkopo wa 3,000,000.

Kikundi hiki kinajishughulisha na kushona viatu, mwenyekiti wa kikundi hiki Rashid abdalla anasema wamefaidika kupitia mkopo huu kwani wanaweza kuhudumia familia zao na kupeleka watoto wao shule.

 Pamoja na mafanikio hayo zipo changamoto mbalimbali ambazo Halmashauri imekuwa ikikabiliana nazo katika suala hili la utoaji wa mikopo ambazo ni pamoja na baadhi ya vikundi kutokurejesha mkopo kwa wakati.

Kwa mwaka wa fedha 2020/2021 halmashauri imetenga jumla ya tsh 159,748,450 kwa ajili ya mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI WA BVR HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA January 23, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • MABADILIKO YA TAREHE YA USAILI September 24, 2024
  • Angalia Vyote

Matukio mapya

  • WWF YAKABIDHI MICHE YA MICHIKICHI KUHIFADHI KINGO ZA MTO RUVU

    May 24, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU NA UWEKAJI WAZI TAARIFA ZA MPIGA KURA AWAMU YA PILI YAFANYIKA KIBAHA

    May 14, 2025
  • WATAALAM WA AFYA PWANI WAKUTANA KUJADILI KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA WATOTO WACHANGA

    May 14, 2025
  • VIONGOZI WA VYAMA SIASA WARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA MKUU WA WILAYA NA MKURUGENZI MTENDAJI KIBAHA DC

    May 07, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Kuzindua bunge
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TOVUTI YA MKOA WA PWANI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA AJIRA
  • TOVUTI YA WANANCHI
  • TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI
  • TOVUTI YA WIZARA YA AFYA
  • TOVUTI YA EWURA

Tovuti Zinazoshabihiana

  • TAMISEMI
  • MKOA WA PWANI
  • TANZANIA
  • AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    KIBAHA DISTRICT COUNCIL

    Anwani ya Posta: P.O BOX 30153

    Simu ya Mezani: +255 23240224

    Simu: +255 0767520048

    Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM)
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.