• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM) |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kibaha District Council
Kibaha District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha

  • Mwanzo
    • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
        • SP FINAL DRAFT
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasmali Watu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Usimamizi wa Sheria
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sehemu ya Mifugo
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Afya ,Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya kisheria
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa halmashauri
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Uchumi na Mipango
      • Maadili
      • UKIMWI
      • Huduma za Jamii
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Dc Kibaha Awakuna Wafanyabiashara Wanaotumia Bodaboda Kusafirisha Mkaa, Awapa Ahueni ya Ushuru

Posted on: May 25th, 2022

Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Sara Msafiri ameshusha ushuru wa maliasili unaopaswa kulipiwa na wafanyabiashara na wabebaji wa mkaa wanaotumia bodaboda maarufu( WAKUBETI ),kutoka 37,500 Hadi 30,000 ili kupunguza utitiri wa tozo zinazowakabili na kuwasababishia kukwepa ushuru kwa kupita njia za panya.

Hatua hiyo imekuja kufuatia Wakala wa Misitu TFS Kibaha kuingia katika msuguano na wafanyabiashara hao ambao wamesusia kupita getini na kuamua kupita vichochoroni kukwepa ushuru ndani ya mwezi mmoja Sasa.

Akiingilia kati mgogoro huo, huko Kwala baada ya wafanyabiashara wa mkaa kugomea ushuru mpya ya sh.37,500 kutoka ushuru wa zamani ya 25,000, Msafiri alilazimika kutoa maagizo manne yanayolenga kujenga mahusiano baina ya pande hizo mbili.

Agizo jingine Ni kuvunja uongozi uliopo wa wafanyabiashara wa mkaa kwa like alichodai umekiuka sheria kwa Kuwa miongoni mwa wanaofanya vurugu na kuisababishia hasara Serikali kutokana na kugomea kulipa ushuru wa Serikali.

Vilevile aliwasihi ,wafanyabiashara hao kuunda vikundi ili vijisajili rasmi na kuanza kulipa kwa mwaka mpya wa fedha kiasi kinachotambulika kisheria sh.361,000 na walipe kwa awamu mbili .

Msafiri alitoa tamko kuanzia sasa kituo kikuu Cha kuuzia mkaa Ni Mlandizi badala ya kuhangaika na pikipiki kwenye barabara kukimbilia soko Mbezi na kwingine.

Mkuu huyo wa wilaya alisema ,hataki kusikia wanakwepa ushuru ,kutumia njia za panya kwani inasababisha hasara kwa Serikali kwa kupoteza mapato mengi.

Hata hivyo alielezea , tozo mbalimbali zilizokithiri 183,000 kwa mfanyabiashara huyu biashara hiyo haimlipi na hawawezi kutoboa kimaisha.

“Tunakimbilia ushuru mkubwa huku walengwa wanakwepa ushuru ,Ni vyema kuweka gharama rafiki ili kuongeza mapato,”;Mwezi uliopita TFS mlipata milioni 38.8 kwa mwezi Sasa mwezi huu mapato yameshuka milioni 24 hiii inatokana na ushuru huu Kuwa mkubwa , na kupelekea msuguano ,”alifafanua Msafiri.

“Nakubali kuvunja sheria,kuingilia Mamlaka nyingine,navunja jongoo kwa meno ,kwa sababu yenu na viongozi mliopo madarakani ,nyie viongozi ndio Daraja Lakini mmegeuka Kuwa wafanya vurugu ,sitokubali nashusha ushuru na nyie mtoke madarakani,kuanzia sasa mchague viongozi wengine”

“Nimesikia hapa mbunge wenu wa Kibaha Vijijini Mwakamo ,alifika hapa mkapanga viongozi na kushauriana viongozi hao wachangiwe fedha waende Dodoma ili kukutana na kamati ya maliasili ya bunge “

Msafiri alisema kwamba ,kwa kushindwa kutekeleza Maamuzi waliojiwekea na Kuwa sehemu ya waliogoma ,nawawajibisha ,na kuanzia sasa wachaguliwe viongozi wapya.

Awali ,WAKUBETI akiwemo Hosea Paulo na Yasin Rajabu alisema , wamekuwa wakichanganywa na Uongozi wa TFS na kusababisha kukwepa ushuru.

“Tunapigwa na migambo , pikipiki zetu zinachujuliwa ,zipo pikipiki Kama 400 huko wanazotubebea na kutulipisha faini ,tozo nyingi zinatuzidia tunajikuta tunapata Faida sh.18,000 Hali hii Ni mbaya,” Kutokana na hali hiyo tunaamua kupeana pikipiki unamlipa mwenye pikipiki ,Sasa hata Kama Ni wewe mkuu utapita getini kulipia au utachepuka kichochoroni !?alihoji Hosea.

Walieleza ,ushuru wa awali ulikuwa 12,500 baadae wakaanza kulipia 25,000 na Sasa Bei kandamizi Ni 37,500 ambayo ni kubwa .

Nae Yasini alibainisha kwamba ,licha ya hayo bei ya shamba nayo ni kubwa 90,000 wakati zamani walilipia 60,000 .

“Mimi Ni mwanaume , familia yangu inahitaji huduma nzuri , huwezi amini mkuu ushuru tunaolipa sisi Ni zaidi ya 180,000 ili kupeleka mzigo sokoni, kwa hali hii ya utitiri wa ushuru hatuwezi kutoboa,Tunashindwa na inabidi kufanya vurugu ili kuweza kujiendeleza kimaendeleo”alieleza Yasini.

Akijibu hoja hizo Meneja wa TFS Kibaha ,Mukama Kusaga alifafanua kila kikundi kilichojisali kina fomu na anaepewa adhabu ni yule ambae hajapata usajili.

Alisema kwa mujibu wa sheria ya misitu na.14 ya mwaka 2002 na kanuni zake mfanyabiashara wa mkaa anatakiwa kulipa sh.250 kwa kila kilo ya mkaa au 12,500 kwa gunia lenye kilo 50.

Kusaga alikiri kuongezwa kwa tozo kutoka 250,000 na sasa 370,000 ambayo imepanda kutokana na hali ya mfumko wa gharama ya kimaisha .

“Tatizo hawabebi gunia moja katika pikipiki wanabeba mzigo mkubwa gunia tatu , Lazima ushuru uongezeke”alisema meneja huyo.

Alisema , kwasasa wapo wafanyabiashara hao 250 ambao husafirisha mkaa kwa kutumia pikipiki na wameshakamata bodaboda 45 na sio 400 na faini ni milioni moja kukomboa pikipiki moja.

Kusaga alikana malalamiko ya kuambiwa wanapeleka mgambo shamba kwenye Misitu na kuwapiga baadhi ya wafanyabiashara wa mkaa , amesisitiza hawajawahi kupeleka mgambo kupiga watu labda iwe mhusika anafanya vurugu.

Wakala wa Misitu wilayani Kibaha ,imeshakusanya milioni 486.7 kutokana na ushuru wa mkaa uliosafirishwa kwa kutumia pikipiki kwa kipindi cha Julai 2021 Hadi Mei 2022, licha ya mapato kushuka mwezi Hadi mwezi kwasababu ya ukwepaji ushuru

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI WA BVR HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA January 23, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • MABADILIKO YA TAREHE YA USAILI September 24, 2024
  • Angalia Vyote

Matukio mapya

  • KAIMU KATIBU TAWALA WILAYA YA KIBAHA ATOA WITO KWA WENYEVITI WA MJI MDOGO MLANDIZI KUZINGATIA UADILIFU

    February 11, 2025
  • MAKAMU WA RAIS AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, ATOA WITO DHIDI YA UBADHILIFU

    April 02, 2025
  • ELIMU YA LISHE JUU YA USINDIKAJI WA BIDHAA ZA VYAKULA YATOLEWA KIBAHA DC.

    March 23, 2025
  • Mwenyekiti wa Halmashauri Amshukuru Rais Samia kwa Fedha za Miradi

    February 05, 2025
  • Angalia Vyote

Video

Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa Kuzindua bunge
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • TOVUTI YA MKOA WA PWANI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA AJIRA
  • TOVUTI YA WANANCHI
  • TOVUTI YA BARAZA LA MITIHANI
  • TOVUTI YA WIZARA YA AFYA
  • TOVUTI YA EWURA

Tovuti Zinazoshabihiana

  • TAMISEMI
  • MKOA WA PWANI
  • TANZANIA
  • AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

Free Visitor&Stat Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    KIBAHA DISTRICT COUNCIL

    Anwani ya Posta: P.O BOX 30153

    Simu ya Mezani: +255 23240224

    Simu: +255 0767520048

    Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Disclamer
    • Maswali ya mara kwa mara (MMM)
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.