WANANCHI WA KWALA WAMEISHUKURU SERIKALI KWA KUWALETEA MRADI WA UMWAGILIAJI MWANGOMOLE
Wananchi wa Kwala wameishukuru serikali kwa kuwaletea mradi wa umwagiliaji ambao kwa sasa upo kwenye hatua ya ukamilishaji.
wananchi wa kwala wametoa shukrani zao hizo wakati ya ziara iliyofanywa na kamati ya fedha uongozi na mipango iliyokuwa na lengo la kuona maendeleo ya mradi unaotekelezwa na Comfix engineering ltd kwa gharama ya 419,000,000/= .
Mradi wa Umwagiliaji Mwangomole Ulianza rasmi mwezi wa pili mwaka 2017 na ulitakiwa kukabidhiwa kwa halmashauri 17/08/2018 lakini haukuweza kukabidhiwa kutokana na changamoto mbali mbali zikiwemo mvua za vuli na masika hivyo wanakatwa asilimia 0.1 kila siku hadi watakapokabidhi mradi huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Mansori Kisebengo amemtaka Mkandarasi anaetekeleza mradi huo kujitahidi kumaliza mradi na kuukabidhi kwani mradi huo umekuwa ukisuubiriwa na wananchi kwa muda mrefu na kuwapelekea kukata tamaa .
pamoja na hayo mwenyekiti anawakaribisha wananchi kuja kufanya kilimo cha umwagiliji kwala kwani mashamba yapo ya kutosha hivyo amewataka watu mbali mbali waje wajiandikishe kijijini kwala ili waweze kupatiwa mashamba hayo.
hata hivyo kamati hiyo ilitembelea ujenzi wa kituo cha afya Magindu na kuridhishwa na kasi ya ujenzi unavyoenda.
kituo cha afya Magindu kilipokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wazazi, chumba cha mionzi na jengo la wagonjwa wa nje( OPD)
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.