NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA AMUAGIZA DC KUCHUNGUZA UJENZI WA MABWENI KWALA.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Tate Ole Nasha , amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kibaha kufanya uchunguzi kwenye mradi wa ujenzi wa mabweni mawili kwenye shule ya sekondari Kwala kwani mradi huo unawalakini mkubwa.
Ole Nasha ametoa agizo hilo baada ya kukagua mradi huo wa ujenzi na kutoridhishwa na mwenendo wa ujenzi huo baada ya kukuta jengo moja halijapauliwa na kuambiwa mbao na mabati havitoshelezi .
Ole Nasha amemtaka Dc kutuma vyombo vinavyohusika kupitia taratibu zote zilizotumika kufanya manunuzi na ikibainika kuna ubadhilifu asisite kuchukua hatua zinazohusika kwa wote waliohusika na ubadhilifu huo.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia amefanya ziara ya kikazi katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha kutembelea miradi inayofadhiliwa na mamlaka ya elimu (TEA) ili kujionea maendeleo ya miradi hiyo.
Shule ya Sekondari Kwala ni mojawapo ya shule zilizopokea hela kutoka mamlaka ya elimu( TEA) kiasi cha tsh 150,000 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili ambayo kila bweni litagharimu kiasi cha tsh 75,000,000,000.
Akisoma taarifa ya ujenzi huo mbele ya naibu waziri, mkuu wa shule ya kwala amesema ujenzi huo unakabiliwa na tatizo la maji kitu ambacho kimesababisha ujenzi huo kutokukamilika kwa wakati.
Vilevile taarifa hiyo imesema vifaa vya jumla ya tsh 17,000,000 vimepungua kwenye ujenzi huo hivyo kumuomba naibu waziri awasaidie kutatua changamoto hiyo ili mabweni hayo yaweze kukamilika kwa wakati.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha amesema amepokea maagizo hayo na atafanya uchunguzi wa kina kwenye mradi huo na endapo atagundua kuna ubadhirifu wa aina yoyote wahusika wote watachuliwa hatua za kinidhamu
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.