Walengwa wa mpango wa TASAF Kijiji cha Kwala wameanza rasmi kuvuna mihogo waliyopanda kama majaribio ya mradi wa kuondoa pengo kati ya walengwa wa mpango na maafisa ugani.
Mradi huu wa majaribio unatekelezwa katika vijiji vitano kati ya vijiji arobain na tano na wanatekeleza kupitia kilimo cha muhogo.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mansour Kisebengo ameshiriki zoezi la kuvuna mihogo katika shamba la walengwa,akiongea baada ya zoezi la kuvuna Kisebengo ameishukuru TASAF kwa kuleta mradi na kuwapongeza walengwa wa mradi kwa kupokea mradi na kuusimamia ipasavyo.
Kisebengo amempongeza Afisa Ugani kwa kusimamia vizuri mradi ambao umeleta matokeo chanya yanayofurahisha.
Mwenyekiti amesema ameona faida ya wataalam kukaa karibu na walengwa hivyo amewaomba wataalam wote kukaa karibu na wananchi ili kuwapa msaada wa kitaalam kwenye mambo mbalimbali yanayohitaji utaalam.
Hata hivyo Kisebengo amewataka wanufaika wa mradi huo kuhifadhi vizuri mazao yao wasikubali kuyauza kwa bei ya chini pia amewataka wahifadhi vizuri mbegu ili mvua zitakapoanza waweze kwenda kupanda kwenye mashamba yao.
Wanufaika wa mradi huo wameishukuru TASAF kwa kuwaletea mradi huo ambao umewanufaisha na kikubwa wamejifunza jinsi ya kulima zao la muhogo kwa faida na pia kuhifadhi mbegu.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.