Mkuu Wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Martin Mtemo amewataka wafanyakazi Wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kufanya kazi kwa weledi na kufuata sheria, taratibu na kanuni.
Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo alipokutana na wakuu Wa Idara na vitengo kwenye kikao cha kujitambulisha kilichofanyika katika ukumbi wa Janga Mlandizi.
Aidha mkuu wa Wilaya amewataka watumishi hao kumpa ushirikiano kwenye utendaji.
Akimkaribisha Mkuu huyo wa Wilaya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Butamo Ndalahwa ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Dc huyo .
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.