KAYA MASKINI KUNUFAIKA NA KILIMO CHA PILIPILI KIBAHA
Wanufaika wa mradi wa kunusuru kaya masikini kijiji cha Dutumi wilaya ya Kibaha wanatarajia, kunufaika na zao la pilipili, kupitia mradi wa PWP, mradi unaotekelezwa na TASAF awamu ya III.
Wananchi hao wamethibitisha kujikita kwenye kilimo cha pilipili wakati walipotembelewa na wajumbe wa kamati ya Siasa wilaya ya Kibaha na kufafanua kuwa, kilimo hicho cha pilipili kitategemea zaidi umwagiliaji na si kutegemea mvua kama hapo awali.
Awali wakisoma wakisoma taarifa ya mradi huo, mbele ya kamati huyo ya siasa, wanufaika hao wameiomba serikali kuwanunulia mashine ya kuvutia maji pamoja na mipira ili kufanikisha mradi wao ambao wanategemea zaidi kuwa, utawakwamua kiuchumi.
Wananchi hao wamesema kuwa wako tayari kuunga mkono kauli ya mhexhimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli ya Hapa Kazi tuu, kwa vitendo huku wakitumia fursa hiyo kujiajiri na kujikwamua kutoka kwenye wimbi la umasikinibwaliokua nao.
Athumani Muhoza.mmoja wa wanufaika hao, amesema licha ya kuwa TASAF inatoa msaada kwa kaya masikini lakini pia ni lazima wanufaika wenyewe kujituma.
"Fursa tuliyoipata ni ya thamani kubwa, na sisi hatutamuangusha rais, tutaendelea kuunga mkono kauli ya Rais Magufuli kwa vitendo, kupitia kilimo hiki cha pilipili" amesema Muhoza
Nae Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini, Murtala Mkumba licha ya kufurahishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri hiyo, ametoa pongezi kwawatendaji wa Halmashauri na wananchi kwa kusimamia utekelezaji wa miradi hasa kwa kuzingatia gharama,Muda na ubora wa mradi.
Aidha amewataka wanufaika hao kujituma kufanya kazi na kuhakikisha miradi hiyo inawatoa kwenye lindi la umasikini waliokuwa nao hapo awali na kuwa wajasiriamali wakubwa katika taifa letu.
Hata hivyo wajumbe wa kamati hiyo wameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi inavyokwenda kwani miradi mingi iliyotembelewa iko katika hatua nzuri za utekelezaji huku miradi hiyo ikilenga zaidi kuwakwamua wananchi kutoka katika umaskini.
Kamati ya siasa Wilaya ya Kibaha Vijijini imefanya ziara ya siku mbili Kwenye halmashauri ya Wilaya ya Kibaha na kutembelea jumla ya miradi 5 ya maendeleo na kujionea namna shughuli za utekelezaji wa miradi hiyo unavyokwenda katika halmashauri hiyo.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.