JAFO APONGEZA UKARABATI WA SHULE YA WASICHANA RUVU
Waziri wa TAMISEMI Mhe, Suleyman Japo ametoa pongezi kwa uongozi wa halmashauri ya wil;ya ya kibaha pamoja na uongozi wa shule ya wasichana Ruvu kwa kusimamia vizuri ukarabati wa majengo ya shule ya Ruvu.
Mhe, jafo ametoa pongezi hizo alipotembelea shule hiyo kujionea ukarabati uliofanywa hivi karibuni na kuridhishwa na ukarabati huo kwani umezingatia vigezo vyote vya ubora na kwa sasa shule inaonekana mpya nay a kupendeza.
Akiongea na wanafunzi wa shule hiyo Mhe, jafo amewataka kusoma kwa bidii kwani mazingira ya shule kwa sasa yanawaruhusu kusoma na kufanya vizuri na kuwaahidi kuwa wakiweza kufaulu vizuri na kuingia katika shule 40 bora Tanzania atawafanyia sherehe kubwa ya kuwapongeza.
Pamoja na hayo Mhe, Jafo alitembelea kituo cha afya Magindu na kukagua ujenzi wa kituo hicho unavyoendelea baada ya kukagua ujenzi huo aliridhishwa na kasi ya ujenzi unavyoenda na kuwashauri waongeze kasi ili kuendana na muda na kuwataka kukamilisha ujenzi huo ifikapo mwishoni mwa mwezi wa kumi.
Wananchi wa Kata ya Magindu wametoa shukrani kwa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, John Pombe Magufuli kwa kuwaletea kituo cha afya kwani wamesumbuka kwa muda mrefu kutafuta huduma za afya na kusema Kituo hicho kikikamilika kitakuwa mkombozi kwa mama wajawazito na watoto.
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.