Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha imeendesha mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo Wahe.madiwani. Mada mbali mbali ziliwasilishwa ikiwemo maadili ya madiwani, kupambana na kuzuia rushwa , mamlaka ya nidhamu kwa mwajiri.Akiwasilisha mada ya maadili ya madiwani Afisa maadili sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Magreth Vulla amewataka madiwani kufuata kanuni na taratibu za maadili ya viongozi wa umma ikiwemo kuvaa kwa stara, kujipamba kwa stara, pia aliwataka wakaongee wanavyoruhusiwa kuongea kwani serikalini sio watu wote wanatakiwa kuongea kuna wasemaji wanaoruhusiwa kuongea kisheria kwa hiyo wakaheshimu hilo.Magreth amewataka madiwani hao wakawe wazi kwenye taarifa za mapato na matumizi ili kujenga uaminifu kwa wananchi waliowachagua.Amewataka pia wakajiepushe na upendeleo kwenye maamuzi wanayoenda kufanya watende haki kwa kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa.Pamoja na hayo amewataka madiwani hao kuweka maslahi yao pembeni na kutanguliza maslahi ya umma na kuepuka mgongano wa maslahi.Mkuu wa dawati la elimu kwa umma wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Fredrick Mbigili amewataka madiwani kukemea vitendo vya rushwa na kuzingatia misingi ya uadilifu na kuacha kupendelea.Mbigili amewataka madiwani hao kusimamia vyombo vinavyotoa haki kama baraza la ardhi kwani hayatendi haki .
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.