DC KIBAHA ASISITIZA MAADILI KWENYE MALEZI YA WATOTO
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe, Yasumpta Mshama amewataka wazazi kuzingatia maadili kwenye makuzi ya watoto kwani wazazi wa sasa wamekua wakisahau kuwafundisha watoto wao maadili yanayofaa.
Mshama ameyasema hayo wakati wakufungua kikao kazi kinachohusu uhamasishaji wa uhuishwaji wa Siku ya Afya ya Jamii na Mabadiliko ya Ufuatiliaji wa Maendeleo na Makuzi ya Watoto Chini ya Miaka Mitano kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa halmashauri.
akiongea wakati wa kikao hicho Mshama amesema halmashauri ya wilaya kibaha imeamua kuhuisha Siku ya Afya ya Jamii iliyokuwa ikitekelezwa miaka ya 1990 chini ya mpango wa UNICEF. Mpango huu ulikuwa unazingatia afya ya watoto chini ya umri wa miaka mitano (5) na ulikazia kuona hali ya lishe ya watoto, chanjo na uliratibu vifo vya watoto ngazi ya jamii.
Mkuu wa wilaya amesema Lengo kuu la mpango huo lilikuwa ni kuwajengea uwezo viongozi wa jamii, kata, vijiji na wataalamu wa afya kusimamia shughuli hizo katika maeneo yao ili kupitia elimu ya afya, jamii ipate uelewa zaidi wa afya ya uzazi na mtoto pamoja na kujikinga na maradhi yanayoambukiza na yasiyoambukiza.
Pamoja na hayo muwezeshaji wa semina hiyo Dk Suleman Kimmata amewataka wamama wajawazito kuzingatia matumizi ya folik acid mara tu wanapogundua ni wajawazito au miezi mitatu kabla ya kubeba ujauzito ili kuzuia watoto kuzaliwa na ulemavu kama vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Vile vile ,Dr Kimmata amewataka Watu wazima na wazee kufanya uchunguzi waAfya zao ukihusisha vipimo vya msukumo wa damu (BP na BMI), hali ya uono, kisukari, kubaini dalili za kifua kikuu (TB). kwa kufanya vipimo hivi mara kwa mara itawasaidia watakaogundulika na matatizo hayo kupata tiba katika hatua za mwanzo za ugonjwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kibaha Bi Ruth Mwelo amewataka wazazi kupunguza hasira kipindi wanapokuwa wajawazito ili kupunguza kuzaa watoto wenye viburi na hasira zilizopitiliza kwani mtoto aliyetumboni anachukua kwa asilimia kubwa tabia za mama.
akichangia mada kwenye kikao kazi hicho Zamda John afisa elimu Taaluma amewataka wazazi kuwalinda watoto katika makuzi yao kwani kwa sasa wazazi wamesahau majukumu yao ya kulinda watoto sababu inayopelekea watoto kuzagaa mitaani na kupata madhara mbalimbali.
washiriki wa kikao kazi hicho wameonyesha kufurahishwa na masomo yaliyotolewa na kuomba masomo hayo yakatolewe kwa watumishi ngazi za kata na vijiji kwani yanamanufaa .
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.