Thursday 28th, January 2021
@Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Anawakumbusha Wananchi Kuwa Mwaka huu 2019 ni mwaka wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Katika Halmashauri yetu na Tanzania kwa Ujumla. Katika Halmashauri yetu Uchaguzi Utafanyika katika Vijiji 26 na Vitongoji 102 hivyo Wananchi Mnashauriwa Mjitokeze Kugombea na Kuchagua Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji Muda Utakapowadia.
Sifa za Mgombea:
1.Awe Raia wa Tanzania
2. Awe na Umri wa Miaka 21 au Zaidi
3. Awe na Uwezo wa kusoma na kuandika Kiswahili au kiingereza
4. Awe na Kipato halali cha Kumuwezesha kimaisha
5.Awe ni mkazi wa kawaida wa eneo la kitongoji
6.Awe ni mwanachama na amedhaminiwa na Chama cha Siasa
7. Awe hajawahi kupatikana na hatia kwa kosa la utovu wa nidhamu, uaminifu au kuhukumiwa
Sifa za Mpiga Kura
1.Awe Raia wa Tanzania
2. Awe na Umri wa Miaka 18 au Zaidi
3. .Awe ni mkazi wa kawaida wa eneo la kitongoji
4. Awe amejiandikisha kwenye daftari la orodha ya wapiga kura
5. Awe hana ugonjwa wa akili uliothibitishwa na daktari anaetambulika na serikali .
KIBAHA DISTRICT COUNCIL
Anwani ya Posta: P.O BOX 30153
Simu ya Mezani: +255 23240224
Simu: +255 0767520048
Barua pepe: ded.kibaha@pwani.go.tz
Copyright ©2017 Kibaha District Council . All rights reserved.